Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abas Kandoro akifungua kongano la Muungano kwa vyuo vya elimu ya juu mjini mbeya leo, kushoto ni Naibu katibu Mkuu Ofisi ya makamu wa Rais Bi Angelina madete,na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya muungano kutoka Ofisi ya makmau wa Rais Baraka Rajab
Waziri wa Nchi Ofisi Ya Makamo wa Rais Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akifafanunua kuhusu masuala ya Muungano katika kongamano lililohusisha vyuo vya elimu ya juu mkoani Mbeya leo.
Washiriki wa Kongamano la Muungano mkoani Mbeya ambao ni wanafunzi wa vyuo ya elimu ya juu wakifuatilia mjadala katika kongamano hilo mjini Mbeya leo.
Ni wajibu wa kila Mtanzania kutambua kwamba uandikishwaji wa katiba mpya unalenga
kuweka misingi ya kuijenga Tanzania ya sasa naya siku nyingi zijazo.
Hayo yameelezwa leo na mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abas Kandoro katika ufunguzi wa
kongamano la vyuo vya elimu ya juu mkoani humo,lililohusu masuala mbali mbali ya muungano
kuelekea maadhimisho ya miaka hamsini ya muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar.
Katika Kongamano hilo Bwana Kandoro aliongeza kwa kusema kuwa jambo hili ni kubwa na
linahitaji umakini wa hali ya juu saana katika kila hatua ili kufanikisha mchakato huu, aidha
Bwana kandoro aliwakumbusha washiriki wa kongamano hilo kuwa Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu nyingi lakini kubwa ni kuwepo kwa mahusiano ya
karibu kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika Nyanja mbali mbali kama vile undugu
wa damu, biashara,utamaduni lugha na mahusiano ya karibu ya kisiasa.
Bwana kandoro aliendelea kusema kuwa, Muundo wa muungano wetu umeweka mfumo
wenye vyombo mbalimbali vyenye mamlaka za utendaji, kutunga sheria na kusimamia shughuli
za umma na utoaji haki.
“Pamoja na hiyo mifumo, na kuwepo sababu nyingi nzuri na za msingi za kuwepo Muungano,
bado ndani ya jamii yetu kuna wanaohoji uhalali wake kupitia maoni yaliyotolewa mbele ya
tume ya mabadiliko ya katiba mahakama na mijadala mingine, alisisitiza.”
Mkuu wa Mkoa alisema kuwa yawezekana kabisa kuwa washiriki wanaweza kuwa na hoja
zinazofanana na hizo..na hivyo mada zitakazotolewa zinaweza kusaidia kujibu baadhi ya hoja.
Katika Kongamano hilo wasomi hao wametoka na kauli mbiu inayosema “MUUNGANO IMARA
NI MUSTAKABALI WA TAIFA LETU.”
Kungamano hili linaondeshwa na Idara ya Muungano ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mikoa
ya Mbeya ya Iringa ni moja ya makongamano katika vyuo vikuu nchini kuelekea maadhisho ya
miaka hamsini ya Muungano
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...