Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akifungua mkutano wa viongozi wa matawi, majimbo na Wilaya kwa Wilaya za Wete na Micheweni uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete
Na Khamis Haji , OMKR
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho wasivunjike moyo na matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki na badala yake waendelee na juhudi za kukiimarisha chama, ili kiweze kukamata dola katika uchaguzi mkuu wa mwakani.
Akifungua mkutano wa viongozi wa matawi, majimbo na Wilaya kwa Wilaya za Wete na Micheweni uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete, Maalim Seif amesema kilichotangazwa Kiembesamaki si matakwa ya wananchi, kwa vile  kimsingi wananchi wa jimbo hilo walisusia uchaguzi huo.
Maalim Seif amesema idadi kubwa ya wapiga kura walioshiriki katika uchaguzi huo si wakaazi wa eneo hilo, ambao walichukuliwa katika maeneo mbali mbali, baada ya kubainika wananchi wenyewe hawatashiriki kwa sababu hawakuridhishwa na maamuzi yaliyochukuliwa hadi kufanyika uchaguzi huo.
“Kama kuna wananchi wa Kiembesamaki waliokwenda kupiga kura basi hawazidi 1000, wengi walichukuliwa katika maeneo tafauti, kama vile Makunduchi, Mtende, Kitope na Bumbwini na wakapelekwa kupiga kura huku wakilindwa na vikosi vya Serikali”, alisema Maalim Seif.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Maalim Seif tafadhali sana epukana na siasa zako za maji taka. Sasa na wewe watu wako walizuiliwa na nani, maana waliopigia kura CUF walikuwa ni chi ya watu 500!!! Au pia kura zako ziliibiwa kama ilivyo nyimbo yako ya maisha yote?
    Wewe ni muumini haya mambo ya kidunia yasikuchafulie imani.

    ReplyDelete
  2. Kauli za Maalim zimezoweleka, hana jipa huyo!!

    ReplyDelete
  3. Kwani CUF walikosa mawakala wa hata kuangalia picha za wapiga kura?

    ReplyDelete
  4. Uchaguzi safi unafanywa Pemba peke yake, Zanzibar (Unguja) hakujawahi kufanyika uchaguzi huru mahali popote!!!!! Si ndio wananchi?

    ReplyDelete
  5. Uchaguzi safi unafanywa Pemba peke yake, Zanzibar (Unguja) hakujawahi kufanyika uchaguzi huru mahali popote!!!!! Si ndio wananchi?

    ReplyDelete
  6. CHA MSINGI NI KUFUATILIA KILA NUNG'UNIKO. KAMA YEYOTE ANAELEZA KUNA TATIZO FULANI BASI NI BORA KULICHUNGUZA KWA UWAZI KABISA BILA MAGUMASHI. KWA HIYO TUSILUMBANE, KAMA AMESEMA KUNA WAPIGA KURA FEKI, TUWATHIBITISHE BILA KUPIGANA VIRUNGU.HUO NDIYO UNAITWA UHURU NA HAKI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...