Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Sokoine ,ambapo alisema maandalizi yote yamekamilika ,majukwaa yamekamilika, uwanja umerekebishwa vizuri na vijana wa Halaiki wamejiandaa vya kutosha tayari kwa sherehe ya kuzaliwa kwa CCM tarehe 2 Februari.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki hatua za mwisho za maandalizi ya mahala ambapo maandamano yatahitimishwa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na vijana wa Halaiki ambao watashiriki kuonyesha Halaiki kwenye kilele cha miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Mbeya tarehe 2 Februari.
Jukwaa litakalotumika kwa burudani likiwa kwenye hatua za mwisho kufungwa kwenye uwanja wa Sokoine ambapo Band ya TOT na wasanii wa vizazi vipya wanategemewa kutumbuiza.
jamani naomba kuliza ccm ilizaliwa tar.2 au tar 5 mwezzi 2 77 sababu hii tar ilikua ya azimio la arusha ikawa tamasha la vijana mpaka ccm sasa naona hapa ina sema tar. 2 feb sielewi naomba mnikumbushe. maadhimisho mema
ReplyDeleteVijana wa "halaiki".....watakaoshiriki kuonyesha "halaiki".....Wadau naomba kufahamishwa maana hasa ya neno hilo "halaiki" na kama ni sahihi kulitumia katika sentensi hizi kwenye hii habari.
ReplyDelete