Mabondia Thomas mashali na Japhet kaseba wamesaini makubaliano ya kucheza  pambano la ubingwa wa mabara wa Universal Boxing Organization (UBO) pambano litakalopigwa tarehe 29 march 2014 katika ukumbi wa Karume hall zamani ukiitwa PTA hall.
 Pambano hilo linaandaliwa na mratibu mashuhuri katika masuala ya ngumi za kulipwa nchini hususani pande za Tanga Ally Mwanzoa alifurahishwa sana kwa nidhamu iliyooneshwa na mabondia hao wakati wa zoezi la kusaini mkataba wa makubaliano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa vijana hall kinondoni yakishuhudiwa na viongozi wa ngumi na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari  kiongozi wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim kamwe aliyefatana na Anthony Ruta amesema makubaliano yamekwenda vizuri na wote wametia saini kupigana pambano hilo litakalopigwa katika uzani wa kilogram 79 na wamechukua malipo yao ya awali kuashiria kuwa pambano hilo lipo na kila mmoja amejigamba kumchakaza mwenzake siku hiyo na kujitengenezea mazingira mazuri katika ubingwa wake huo.
Mabondia Thomas Mashali (kushoto) na Japhet Kaseba na promota wa pambano baada ya kusaini makubaliano ya kucheza  pambano la ubingwa wa mabara wa Universal Boxing Organization (UBO) pambano litakalopigwa tarehe 29 march 2014 katika ukumbi wa karume hall zamani ukiitwa PTA hall.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...