Washiriki wa maisha Plus wakichimba shimo kwa ajili ya kujenga choo cha shule ya msingi Igula.

 Baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus 'Rekebisha' wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya kazi ya kuchumba matundu ya choo katika shule ya msingi Igula tarafa ya Ismani mkoani Iringa kulikokuwa na kijiji cha awali cha mashindano hayo.
 Baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus 'Rekebisha' wakiwa wamepumzika baada ya kufanya kazi ya kuchimba matundu ya choo katika shule ya msingi Igula tarafa ya Ismani mkoani Iringa kulikokuwa na kijiji cha awali cha mashindano hayo.
 Moja ya nyumba za watu wasiojiweza ikiendelea kukarabatiwa na washiriki wa maisha plus 'Jirekebishe'
Baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus 'Rekebisha' wakigawana chakula.


MAISHA PLUS ‘REKEBISHA’  WASHIRIKI KAZI ZA JAMII

Na Denis Mlowe,Iringa

WASHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus walioko katika kijiji cha awali cha Igula kilichoko tarafa ya Ismani kata ya Kihorogota wameshiriki katika kazi za kijamii zikiwemo ujenzi wa choo katika shule ya Msingi Igula.

Washiriki hao 20 wakiongozwa na mwenyekiti Yasinta Hokororo wamefanikiwa kukarabati baadhi ya nyumba ambazo zinakaliwa na wazee wasiojiweza na kufanya shughuli za kilimo kwa walezi wanaoishi nao kijijini hapo.

Akizungumza,Hokororo alisema maisha wanayoishi kijijini hapo ni kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kijiji ikiwemo kuwasaidia wazee wasiojiweza kuwahudumia shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo.

Alisema changamoto wanazokutana nazo zimewafanya kuwa mahiri katika utendaji wa kazi tofauti na maisha yao ya nyumbani.

Hokororo alisema maisha wanayoishi katika kijiji cha awali lengo kuu ni kurekebisha changamoto wanazokumbanazo wananchi wa kijiji husika zikiwemo za kilimo kwa kuwapa mbinu mbalimbali za kujikwamua na kupata mazao bora.

“Moja ya Changamoto ambazo tumekutana nazo hapa ni masuala ya kilimo na wanafunzi wa shule ya msingi Igula kukosa choo bora hivyo sisi kama vijana tukaamua kuanza na ujenzi wa choo kwa wanafunzi hao na kisha kwenda mashambani kusaidia kazi za walezi wanaotulea.” Alisema Hokororo

Kwa upande wake mkuu wa usanifu wa Maisha Plus Kaka Bonda alisema shindano la mwaka huu limekuja na kauli mbiu ya ‘Maisha Plus 'Rekebisha’ likiwa na lengo la kuingia ndani ya jamii na kuibua na kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo na kuzitatua kwa njia mbadala.

Bonda alisema washiriki wa  shindano hilo watakuwa na jukumu la kufanya kazi za kijamii zaidi na kuwasaidia watu wasiojiweza katika maisha ya kijijini na kurekebisha baadhi ya vitu ambavyo kwa namna moja au nyingine wanakumbana nazo.

“Kama unavyoona vijana wameanza kutengeneza choo cha shule ya msingi Igula, na wanaendelea na ukarabati wa nyumba ya mzee asiyejiweza baada ya kuanguka na mvua ndio kazi ambazo kwa mwaka huu wa maisha plus rekebisha watahusika nazo washiriki.” Alisema Bonda

Alisema shindano la mwaka huu litakuwa la kimataifa zaidi kwa kushirikisha washiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Tanzania.

Alisema maisha plus kipindi cha televisheni kinachoonyesha maisha halisia ya Vijana na Wakulima Wanawake ambao ni mama shujaa wa chakula hivyo washiriki wanaohitajika kuingia katika fainali ni 9 kati ya 19 walioko katika kijiji na kisha wataelekea kijiji cha awali cha Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...