Mshindi wa shindano la Mama shujaa wa chakula mtandaoni, Neema Urassa Kivugo jana alikabidhiwa zawadi ya shamba la hekari 10 alilochagua kwa ajili ya shughuli za kilimo. 

Neema Urassa Kivugo ambaye alishinda vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. Milioni 5 alichagua kununua shamba ili amiliki ardhi yake mwenyewe. Akiongea wakati wa makabidhiano hayo, Neema alisema, ''kupitia kilimo katika shamba langu mwenyewe, sasa nitaweza kumalizia ada ya wanangu na pia ujenzi wa nyumba yangu kwani sasa sikodishi tena shamba". 

Mama Shujaa wa chakula mtandaoni ni shindano lililoandaliwa na kuratibiwa na balozi wa kampeni ya Grow Shamim Mwasha. Shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa mwaka 2013, liliwataka wakazi wa mijini kuwapendekeza ndugu zao ambao ni wakulima wanawake wanaojishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula kwa ajili ya kushinda vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. milioni 5.

Akielezea kuhusu kampeni ya GROW katika makabidhiano hayo, Mkamiti Mgawe ambaye ni afisa wa kampeni, ushawishi na utetezi kutoka Oxfam alisema Grow ni kampeni ya kimataifa inayoratibiwa na Oxfam yenye lengo la kuhakikisha kwamba kila mmoja ana chakula cha kutosha kila siku"

Neema Urassa Kivugo kutoka Kibaya Kiteto mkoani Manyara aliibuka kidedea kwa kupata asilimia 76.95 ya kura zote.

Mama Shujaa huyo pia amejishindia nafasi ya moja kwa moja ya kushiriki katika shindano kubwa la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika sambamba na kipindi cha maisha halisia cha Maisha Plus ambalo linatarajiwa kuanza kuonekana kwenye televisheni kuanzia mwezi Machi mwaka huu.

Mama shujaa wa chakula mtandaoni ilifanyika kupitia blogs za 8020fashions, Millard Ayo, Michuzi Blogs, Blog za mikoa na Missie Popular blogs. 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...