DSCF2464Mbunge viti maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine akiwasili katika viwanja vya kituo cha huduma ya walemavu cha kanisa katoliki jimbo kuu Arusha,Monduli jana kwa ajili ya kugawa misaada mbalimbali.
 DSCF2485Mbunge wa Viti maalum Namelok  akimjulia hali mtoto mwenye ulemavu wa utindio wa ubongo kituoni hapo.
DSCF2533
Namelok akikabidh msaada huo kwa Mratibu wa kituo cha watoto walemavu Monduli,Bi Mireile Kapilima.
DSCF2517Katibu wa UWT Mkoa wa Arusha Stamili Dendegu akimuendesha mtoto mwenye ulemavu wa miguu kituoni hapo
DSCF2515Walemavu wakiwa katika baiskeli zao wakimsikiliza Mbunge Namelok

Na Pamela Mollel,Monduli.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine ameitaka jamii kujitolea kuwasaidia watoto walemavu wanaolelewa katika kituo cha huduma ya walemavu cha kanisa katoliki jimbo kuu Arusha kwa kuwa wazazi wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu
Alisema hayo jana wilayani Monduli wakati akikabidhi misaada mbalimbali huku akiungwa mkono na wanawake wenzake waliomsindikiza kuwaona watoto wenye ulemavu wa viungo na utindio wa ubongo
Namelok alisema kuwa kuna baadhi ya wazazi ambao hawana uwezo wa kumudu kulipa shilingi 1500 kwa siku hivyo ni vyema jamii ikaguswa kuwasaidia watu wenye uhitaji
“Zipo familia zinatumia zaidi ya  shilingi 1500 kwa siku kila mmoja akijitolea itasaidai kwakuwa kwa mwezi ni shilingi elfu 45000 kwa mtoto mmoja”alisema Namelok
Pia mbunge huyo alitoa shukrani zake kwa Mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa kwa kuweza kutoa eneo hilo  na kujengwa kituo chenye uwezo wa wawahudumia watoto 52.
Misaada aliyokabidhi Mbunge huyo ni pamoja na Blanket 50, shuka,unga,mchele,sabuni,sukari na mafuta
Mratibu wa kituo hicho Mineile Kapilima alisema kituo hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali  ikiwemo ukosefu wa ufadhili wa kudumu hivyo mahitaji  ya kituo kuongezeka siku hadi siku kwa kuwa awali kituo kilikuwa kunauwezo wa kulaza wototo 30 lakini kwa sasa wanafika hadi 52
 “ukosefu wa chakula,matibabu,nguo,hatuna ufadhili wa kudumu kwa kuwa wazazi wengi hawana hawana uwezo”alisema  Kapilima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...