Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. JK hao wajumbe tayari wameshakuwa wa upande mmoja, kwa miaka mingi sasa serikali imekuwa ikiendeshwa kwa kunufaisha sio watanzania ila watanzaniawakirisito huu ni ukweli huwezi kuupinga , na hata hao wajumbe wengi wameingia kwa njia tofauti kupitia NGO nk kinyemela watavutia upande wa dini yao, jambo hili ni muhimu ili kuzuia mvutano huko mbele , tanzania ni ya watu wote na makabila yote, rangi dini au jinsia si vyema kwa ndugu zetu wakisto kuona kuwa hii ni nchi yao peke yao , hivi karibuni tu nimeona wameingilia masuala ya ardhi , huu upendeleo JK unabidi uachwe na kama huuamini basi fanya tathmini utapata jibu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha mawazo ya udini,hakuna nchi iliyoendelea kwa wananchi kuwa na fikra kama hizo hasa kwa mambo muhimu kama haya.

      Delete
  2. Mh JK watanzania hawasomi.Angalieni mchakato wa bunge la waingereza wanavyopata sheria mswaada unasomwa neno kwa neno,msitari kwa msitari. na mswaada unaweza kurushiana house of Lords na house of commons kwa mara nyingi sana watanzania hawasomi,wabunge hawasomi na ndo maana wanaharibu sheria.hapo kuna kazi nzito.Hatuhitaji kupeleka ubishi usio na masilahi kwetu watanzania.wabunge jifunzeni busara za Raisi wetu JK.MDAU uk

    ReplyDelete
  3. unatuchafulia hali ya hewa na hadithi za udini hapa. Ongea mambo ya manufaa kwa taifa acha fikra finyu

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza ana upeo mfupi sana wa kuelewa mambo. Uelewa wake katika dunia hii ni dini. Watu tunasema kila siku kuwa tuachane na fikra finyu zenye mwelekeo wa udini, mwenzetu hayamwingii kichwani mwake hayo. Anakuja hapa na kuibuka na hoja za kidini.
    Nina muomba aisikilize tena na tena na kwa makini hotuba ya Mhe. JK. Ni shule kamili kwa kila mmoja wetu wenye nia ya kutaka kueleweshwa mambo muhimu kama haya ya Katiba ya nchi yetu.
    Ahsante sana Mhe. Rais wetu. Umenena kweli kabisa.
    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  5. Kuna watu wametuomba watanzania tuwe Tunasifia .
    Nifikishie salaam zangu za pongezi kwa Mr Prezdent Jakaya M Kikwete kwa mawazo yake mazuri na kutowa ruhusa ya kujenga katiba kwa amani na upendo ili tufikie malengo.
    Kazi imebaki kwa wawakilishi wetu msituangushe,mkabaki mnazozana na kutopata jawabu la mzozo.
    Nchi inajengwa kwa mawazo ya pamoja ya kujenga nchi bila kujali vyama dini rangi wala kabila.
    Tanzania kwanza.

    ReplyDelete
  6. nakubaliana na mdau namba moja tanzania yetu imebeza upande mmoja kidini tusikatae tufanye utafiti halafu ndio tupinge , serikali inatumia bilions za fedha kama ruzuku au misamaha ya kodi kwa taasisi za kikristo tu wakati nchi yetu ina dini nyingi katika hizo mbili ndio kuu, kiasi mumpigie debe JK kwa kuwa amekupeni ulaji nje nje , wala sio kweli kama wadau wengine hapo juu wanavyobisha kijazba , kaangalieni kila sehemu ya serikali kuanzia ngazi ya chini mpaka juu hakuna uwiano kidini , hicho ni kitu muhimu ikiwa tinataka kuishi kwa utulivu ndugu zangu , msikatae upendeleo uliopo , mimi sisemi kuwa dini nyengine zipendelewe ila kuwe na usawa , asanteni kwa kusoma maoni

    ReplyDelete
  7. Mfume-dume naona unaonekana maana sioni kina mama wengi ktk mkutano huu wakati waume kwa wake tupo asilimia 50 kwa 50 katika uwiano wa idadi ya watu Tanzania.

    Masuala ya kidini takwimu hazifahamiki na ziendelee kuwa hivyo, mtu apate nafasi kwa kuangalia ana vigezo vinavyotakiwa kwa nafasi yoyote ile iwe ajira, nafasi za masomo n.k

    Mdau
    Mfumo-Kike

    ReplyDelete
  8. Jamani tuwe watu wenye utu kweli na watu wa kumwogopa Mungu wakati mwingine tunapowasirisha hoja zetu. Tanzania haina udini kabisa. Na kama udini ungekuwepo mpaka leo tungekuwa tunaongelea kulipiza visasi vya mauaji ya padre na kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa Kikristo huko Zanzibar. Hakuna udini ila ninyi mnaoongelea suala la udini hapa ndo mnataka kuleta utengano kidini. Si vema kusema kitu usichokuwa na data zake. Ni ushauri tu

    ReplyDelete
  9. Watoto wadogo ndio hao wanaosema maneno hayo ya kuwa hakuna udini ila kinyemela upo, ila hao wazee wao wanajua ukweli kwenye hayo, Na hapo juu wanaosema hakuna ukristo kupeta hawajafanya uchunguzi,
    Wasiende mbali sana kwa kuwasaidia tu kidogo waanzie miaka ya nyuma kidog kwenye mfumo mzima wa elimu, huu ndio mfumo mama wa kila kitu wa nchi, ilikuwa vipi, ndio maana Leo unaona hakuna uwiano kwenye mgawanyo wa madaraka, misamaha na mapunguzo ya kodi kwa pande moja.
    So when u talk....first,back to the reseach, then come straight forward to the ground..
    Sasa I dought kitu kimoja isije kuwa wakaja na other face katika hilo ili ku-penetrate katika misingi lie ile waliyoazimiana.
    Watambue hii nchi yetu wote, tuishi kwa misingi ya usawa na kuheshimiana na wazi hasa na mambo ya nchi.
    Otherwise siku moja tutajuta sote kwa pamoja. Maana hakuna nchi nyingine inayoitwa tanzania zaidi ya hii.
    Kama suala linakuwa gumu sana na halina ufumbuz ni bor kuggawana nchi mie wazo langu, ili kuondoa kelele hizi wanazo dhani.
    Busara ipewe kipao cha mbele kwenye hiyo katiba kuipitisha.
    Shukran sana ,mh jk. Kwa utangulizi.
    Mungu ibariki tanzania.
    Mdau.dsm

    ReplyDelete
  10. Kuna-watu hupenda kuandika comment za udini ili kutafuta uoga wa watu kwenye haya maswala muhimu kwenye hili, la taifa letu. na tunawajua ni watu gani, Tanzania tuna waamini viongozi wetu na wanapokua kwenye madaraka huwa wanafanya kama taifa linavyotaka. sikliza vizuri hotuba ya Mh.Rais j kikwette.

    mdau holland.

    ReplyDelete
  11. Inasikitisha, inasikitisha, inasikitisha!
    Ukiishiwa na hoja, na bado ukataka usikike, hakika unakuwa adha hata kwako wewe mwenyewe binafsi. Sikia rafiki: Sheikh Mkuu hivi karibuni kayasemea haya haya, na nikadhani limeeleweka kwa waumini, kumbe bado wapo wachache ambao ama hawajaelewa, ama wameelewa lakini hawataki kukubali ukweli, na kuwajibika bila kulaumu wengine! Sikiliza rafiki; kama kungekuwa na ubaguzi wa dini katika nchi hii kutoka kwa wakristu, kama unavyo-imply, basi nakuomba uanze kujiuliza, hasa kama una umri mpevu kidogo, ati kwanini basi Mwl Nyerere alitaifisha zile shule za mission, punde tu baada ya Uhuru, na kuziweka ziwe za serikali? Haya, oil-dollars nionazo zikiingia Tanzania kila uchao tangia siku nyingi tu, ziko wapi bali zimewekezwa everywhere, but in education!
    On the other side, rafiki yangu hebu nenda leo kwenye shule yoyote ile ya mkristu binafsi, ama hata hadi vyuo vya tertiary education vilivyo chini ya Taasisi za dini za kikristu, kama hutakuta wanafunzi wa dini zote, kwa raha na uhuru wao kamili, wamedahiliwa na wanasoma! Lakini jambo na ishara muhimu zaidi (very symbolic and significant) ni uamuzi alioufanya Rais B.W.M. wa kukikabidhi kilichokuwa Chuo Cha Tanesco pale Morogoro, tena buuureee, ili kichangie elimu. Sote watu wazima tuliona lile lilikuwa jambo la kijasiri sana, na jema sana, tena naweza kusema ilikuwa THE STATEMENT! Kwa ambao hawakuonekani kama hata walikuwa na punje mioyoni mwao ya kuthanimi hatua hiyo ya, yet another Statesman - BWM, basi hutajua hata ufanye nini waone unavyojali! Hakika ujue, wanaojua na kuthamini elimu kamwe hawataacha kusomesha watoto wao ili ati basi wote tufanane! Ng'o, hilo utalisubiri sana, wakati wenzako wanaongeza kasi.
    Sasa, ukisikia mtu, tena wa kiwango cha 'informed society', anafikia hatua ya kupaaza sauti akifanya utatuzi rahisi kwa kutofanikiwa kwake na kusema; "Tugawane nchi", utaachaje kupaaza sauti nawe, tena kwa kumshangaa kweli kweli, ukisema; Inasikitisha, inasikitisha, inasikitisha!

    Ndugu mhariri, hebu niruhusu niongeze tena machache tuyaonayo sote Watanzania. Jamani eeh, huyu Rais wetu wa sasa naye kajitahidi kweli kusisitiza kwamba watu wasome pia elimu dunia, lakini mafanikio yanakuja siyo kwa kasi ambayo mtu ungetumaini.
    Sikiliza rafiki, hapo middle-east, ambako ndiko kulianza hizo dini zote tunazozigombanisha hapa Tanzania, wanasoma kweli kweli elimu dunia, kama tu wanavyosoma vitabu vyao vitakatifu. Sisi ndiyo tutajiteteaje?
    Well, mimi natoka familia, na ukoo, unaoundwa na waumini wa dini zote, na nikwambie ninamshukuru Mungu kwa mafanikio aliyo tujaalia. Najua hilo ilikuwa ni kwa sababu wazazi wetu walitupeleka shuleni pia. Mimi binafsi nilisoma Madrasa na katekisimu, na wala sijawahi kudhani kwamba hilo lilikuwa jambo la kunitenganisha na ndugu zangu ambao tulija chagua kuendeleza uchaji wetu wa Mungu kwenye majengo tofauti!
    Inasikitisha, inasikitisha, inasikitisha saaana!
    Lini utawapenda wenzio na kuwaamini kama wanavyokupenda na kukuamini wewe!?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...