Na Francis Godwin, Iringa 
MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (48) leo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Iringa akituhumiwa kwa kosa la kujeruhi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli. Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elizabeth Swai alisema Mchungaji Msigwa alitenda kosa hilo Febrauri 5, 2014 katika kijiji cha Nduli, mjini Iringa.
 Alisema Mchungaji Msigwa anashitakiwa kwa kumjeruhi Salum Kahita kinyume na kifungu kidogo namba 225 cha sheria ya kanuni za adhabu. 
Akiwa amefunguliwa kesi ya jinai namba 28 ya mwaka 2014, Mchungaji Msigwa anayetetewa na wakili Lwezaula Kaijage alikana kosa hilo na hakimu aliahirisha kesi hiyo itakayotajwa tena Machi 10, mwaka huu kwa kile kilichoelezwa kwamba uchunguzi wake haujakamilika. 
Pamoja na Mchungaji Msigwa, jeshi la Polisi limewapandisha kizimbani Meshack Chonanga (22) na Paulo Mapunda wote wakazi wa kijiji cha Nduli mjini Iringa wakituhumiwa kumjeruhi Alex Mpiluka wakati wa kampeni hizo.
 Watuhumiwa hao walirudisha mahabusu ya mahakama hiyo baada ya wadhamini wao kuchelewa kufika mahakamani hapo. Kama ilivyokuwa kwa Mchungaji Msigwa, nao kila mmoja anatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaoweka dhamana ya ahadi ya Sh Milioni 2.
Akitoka mahabusu ya mahakama hiyo
Akiwasalimu wafuasi wake

Ndani ya mahakama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. yaani inaonekana kwa hichi chama kwao ni ujiko kila siku wwkamatwe waachiwe waandikwe mheshimiwa msigwa jimbo lako lina matatizo mengi yatatue kwanza sio kila siku ww tu mbona hatuskii mnyika hatuskii zito kabwe hatuskii kuna yule wa karatu ww tu na lema

    ReplyDelete
  2. The mdudu,,jamani nyie waheshimiwa ndio mnaotakiwa muwe mfano kwa jamii yetu,,la sivyo hatutojifunza chochote toka kwenu hii ni aibu sn

    ReplyDelete
  3. Hivi Mhe. Mchungaji Msigwa wewe ni Padri ama ni Bondia?

    Jamani nashindwa kuelewa pana uhusiano gani kati ya Upadri, Siasa na Ubondia?

    Inaelekea Siasa imesha kushinda!

    ReplyDelete
  4. Hizi mahabusu ziboreshwe. Juzi juzi jamaa yetu kawekwa mahabusu huko kanda ya ziwa mpaka kalazimika kunywa maji machafu. Mtu anapokuwa mahabusu ni mshukiwa hivyo si vizuri kumyima kunywa dawa zake kama huyu mzee alivyonyimwa kuwa na dawa za kisukari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...