Kikundi cha wake wa Viongozi (Mellinium Women Group) yatoa msaada wa Chakula, Mavazi na Vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. Milioni 6.8/- kwa “New Hope for Girls Organization’’ kinacholea wasichana wanaoishi katika mazingira magumu.

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda alieleza kuwa, wake wa viongozi waliguswa baada ya kukutana na Bibi. Consoler Eliya mwaka jana katika mkutano wa wanawake wajiwezeshe kiuchumi ambaye ni miongoni mwa wasichana walioishi katika mazingira magumu na kuahidi kumsaidia.  

Misaada hiyo ilitolewa jana mchana (Ijumaa, Februari 7, 2014) kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay, jijini Dar es Salaam

“Wakina mama wameona jitihada za Bibi. Consoler katika kusaidia wasichana hawa wanaoishi katika mazingira magumu, ambayo watu wengi wamekuwa wakiyapitia na kushindwa kujitolea kama ilivyokuwa kwa Bibi. Consoler’’,alisema.

Mama Pinda aliongezea kuwa, nia ya Serikali ni kuhakikisha watoto husasani wakike wanaishi kwa amani na kupata haki zao za msingi kwani maisha yao yamekuwa ya huzuni kubwa mno.

Baada ya makabidhiano hayo, Bibi Consoler Eliya, aliwashukuru sana wake wa viongozi kwa msaada waliotoa: “mhitaji si lazima awe yatima, mhitaji anaweza kuwa na wazazi wote na bado akawa anaishi katika mazingira magumu hivyo sisi tunaishi na watoto walitoka katika makundi tofauti ya mazingira magumu’’ alisema.

Mbali na kulelewa katika kituo hicho, pia wasichana hao wanabuni na kutengeneza vitu kama batiki, mikufo ambayo inasaidia kuendesha maisha yao, aliongezea Bibi. Consoler.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Mama Lukuvi aliongezea kuwa, kutokana na juhudi zinazooneshwa na wasichana hao  Kikundi kitawawezesha meza katika mkutano wa wajasiriamali utakaofanyika hivi karibu Jijini Dar es Salaam ili waweze kupeleka bidhaa zao za ubunifu wanazozitengeneza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...