MHE. Murtaza Mangungu(MB)Kilwa Kaskazini akiwa na Bwana Phanuel Ligate (Mwakilishi wa Diaspora) Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma November 2012

Habari za Wakati huu ! Nimekuwa nikifuatilia mijadala na maoni mbalimbali kupitia mitandao na wengine walionitumia e-mail au kunipigia simu. 
Kwa Kuwa mawasiliano yetu hayakuwa bayana nilidhani nitoe ufanunuzi kuhusu suala la uraia pacha (Dual citizenship ) . Awali ya yote Naomba radhi sana ikiwa maelezo ninayotoa nitamkwaza yeyote ila naomba iaminike si kusudio langu, pengine ni uelewa na nitakuwa tayari kukosolewa.
Nawapongeza sana kwa jitihada kubwa mnazozifanya ili kufikia lengo , nawahakikishia Kuwa nitakua wa mwisho kukubaliana na suala hili kutoingizwa kwenye katiba mpya. 
Binafsi naelewa kila neno mnalomaanisha na faida ya kuwapo kwa 'dual citizenship " kwa faida ya nchi yetu na ustawi maridhawa wa jamii zetu kwa ujumla.
Ukisoma katiba yetu ya sasa na rasimu ya katiba mpya hakuna kipengele ambacho kinazungumza Aina ya uraia na pia hakuna tafsiri ya Raia ni ipi . Ibara ya ya katiba ya Mwaka 1977 kifungu 13(1)(3) ,17(1), 22(2), 28(1), 29(1)(2)(3) zimetamka Raia bila kutafsiri 'Raia" ni nani.
 Aidha kwenye vifungu au kwenye jedwali la tafsirihttp://www.katiba.go.tz/. Rasimu ya katiba ya 2013 Ibara ya 38 imetamka ya uraia bila ya kutoa kwa ufafanuzi 'Raia " ni nani au aina za uraia. 
Ukisoma sheria ya uraia ya Mwaka 1995( The Tanzania Citizenship Act, 6 of 1995 )http://polis.parliament.go.tz/PAMS/docs/6-1995.pdf ndipo unapata tafsiri zote kuwa raia wa Tanzania ni nani na aina zipi za uraia kwa mujibu wa sheria. Kimsingi aina za uraia ama 'Dual Citizenship " si suala la kikatiba bali ni sheria ya Uraia . 
Zipo jitihada kubwa za kiushawishi kutoka kwa Mh. Rais Dr. Jakaya Kikwete , Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe pamoja na viongozi wa Sekretarieti ya CCM (Mh. Madelu Mwigulu Mchemba na Ndugu Nape Nnauye) Kuwa lazima suala hili lipewe kipaumbele na msimamo wa chama 'CCM" ni Kuwa lazima pawepo na haki hii ya uraia pacha.

Zipo namna mbili za kuwasilisha hili kwenye Bunge la katiba

I. Kupeleka jedwali la mabadiliko ( schedule of amendment )
II. Kupeleka mabadiliko ya kifungu kwenye Kamati ili iwasilishwe bungeni kwa mjadala.
Binafsi nimeamua kutumia njia zote ili kuhakikisha hakuna mkwamo. Nawashukuru sana wale wote walioniagiza nihakikishe suala hili nalisimamia ipasavyo , Ndugu Iddy Sandaly, Alhaj Kalala , Ndugu Phanuel Ligate , Richard Mwandemani ,Khalfani Lyimo na wengineo wengi. Ninawahakikishia Kuwa nitalisimamia jambo hili kwa kadiri ambavyo Mungu ataniwezesha. 
Siwezi kusahau hata kidogo maisha ya wema niliyoishi na wenzangu huko ughaibuni , pia hakuna namna itakayonifanya nisahau umuhimu wa jambo hili ikiwa binafsi ni miongoni mwa ' wahanga'' wa janga hili

Ahsanteni
Murtaza Mangungu(MB)
Kilwa Kaskazini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. God bless you Hon. Murtaza mangungu.

    By:
    Ambassador H. K. Saudin

    ReplyDelete
  2. Kaka M.Mangungu hongera saaana kwa jitihada zako, tunakuombea mungu akutangulie na akujalie wepesi wa jambo hilo jema unalowatakia ndugu zetu waishio ughaibuni. Mimi mwenyewe niliishi ughaibuni kwa mda mrefu nikaamuwa kurudi baada ya mkataba wangu kumalizika, lakini hadi sasa najuta kwa nini sikuomba uraia maana unafaida zake, kama vile uhuru wa kusafiri duniani kote kwa mda ninaotaka mimi, lakini sasa nikitaka kutoka nakutana na mizengwe ya visa hadi unakata tamaa. Ukiritimba umejaa katika nchi zetu za kiafrika hadi unakuwa kero. Wana Diaspora nawaomba wawe watulivu wawe na subira hadi kieleweke, na mungu yuuu pamoja nanyi najuwa ni haki yenu kuwa na uhuru katika nchi yenu lakini utawala wa kichoyo na ubinafsi ndio umejaaa nchini mwetu, Mdau wa hoja ya haja. AHSANTENI

    ReplyDelete
  3. Mimi nauliza hao wanaokataa wanasababu zipi zinazowafanya kukata .Mbona Wazungu, wachina na wakenya wanaoa dada zetu na kupewa uraia wetu bila ya kuambiwa kuwa waukane uraia wa kwao?

    ReplyDelete
  4. Hongera mh, Mangungu. Ubarikiwe na Mungu, tupo pamoja.
    Mdau Chiberia-Chitown.

    ReplyDelete
  5. Hakuna haja ya uraia pacha. Wazawa wapewe ukazi wa kudumu watakapohitaji kurudi bongo.

    ReplyDelete
  6. Ahsante sana Mhe. Mangungu.

    Ukweli wa mambo hili suala la Uraia Pacha linapata Wapinzani na Waungaji mkono kwa vile LINA FAIDA na HASARA ZAKE.

    Ni kama ilivyo ktk Economics pana 'Opportunity costs' and 'Sacrifice costs'.

    Kiuchumi na Maendeleo Madiaspora wana faida lakini tukija ktk upande wa pili wa Sarafu tunakuta vitu kama Usalama wa nchi ukizingatia wengi wa hawa ndugu zetu walisha asi kwa Kuukana Uraia hivyo moja wa moja hili linawapa wakati mgumu kuaminiwa na engi wanao pinga Mpango huu.

    Nionavyo mimi ili ku-balance mambo ni bora Tanzania turekebishe Sera zetu 'POLICIES' zetu hasa ktk yale maeneo ambayo yanawabana ndugu zetu hawa Madiaspora ili waweze kushiriki nasi hata kama watakuwa na STATUS ZAO ZA HUKO WALIPO.

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  7. Hatuwezi kuingia ktk Ukoloni Mamboleo kwa ku-'Copy and paste' kila ambacho nchi zingine duniani zinafanya kama kuukubali huu Uraia Pacha!

    Tukumbuke hii ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio Rwanda, Uganda ama Kenya ambako wamekubali suala hili kwa sababu zao wao na sio iwe sisi.

    Hakuna Utumwa mbaya ktk maisha ya binaadamu wa kuishi ama kuendesha mambo kwa kufuata mkumbo, ama kuishi maisha ya wengine badala ya kuishi maisha yetu kama Tanzania.

    PASIPOTI MOJA MTU MMOJA NA SIO PASIPOTI MBILI MTU MMOJA!

    ReplyDelete
  8. Hawa jamaa Madiaspora mimi nawachukulia kama Waasi wakubwa ama Wahalifu.

    1.Ni kwa sababu, wengi wameondoka nchini wakidai eti ohhh Tanzania nchi ya shida.

    2.Wengi wameipakazia sana Tanzania ili kufikia malengo yao huko, wapo walio diriki kudai ya kuwa wamekanamizwa na Serikali hiyo hiyo ya Tanzania wanayoitaka leo iwape Uraia Pacha.

    3.Wapo walioondoka kwa sababu halali kama Masomo ama Kikazi lakini cha ajabu baada ya muda wa sababu zao hizo kwisha wakaendelea kukaa huko bila sababu yeyote ama umuhimu huku wanacho kifanya kikiwa hakieleweki wengine wakidaiwa kuishi kwa kufnya Uhalifu na kuichafua Tanzania.

    Jambo linguine gumu ni kuwa wengi wanao pigia chapuo za Uraia Pacha azma yao kubwa ni kuwani Uongozi nchini Tanzania.

    UONGOZI UNATEGEMA SANA MSIMAMO WA MTU HASA KWENYE SUALA LA UZALENDO NA NIA NJEMA KWA NCHI NA WANANCHI.

    SASA HEBU WAJAMENI TUTATHIMINI, ITAKUWA IMEKAAJE TUJE KUPATA KIONGOZI TANZANIA MBAYE ALIWAHI KUASI NCHI KWA KUUKANA URAIA?

    ReplyDelete
  9. Msiwe na tamaa ya kutaka huko na huku.

    Kuweni na Uraia wenu huko na sisi tubaki na Pasipoti yetu moja ya Uraia wa nchi moja ya Tanzania.

    Tutakuwa tuna tembeleana tu inatosha sana.

    Bakini majuu kwenu huko muendelee na maisha yenu na sisi tubaki Tanzania na lwetu!

    ReplyDelete
  10. Viongozi wetu wanaoendeleza hii agenda ya uraia wa nchi nyingi wanalichukulia swala la kuwapatia umaarufu wa kisiasa. Tukiruhusu hili jambo, hata raia wa kigeni wataomba uraia wa Tanzania. Watapata haki ya kumiliki ardhi na fursa nyingine ambazo mtanzania wa "kuzamia" hupati ukiwa huko ughaibuni. Kama uliona ulaya ni pazuri iweje leo hii unaona Tanzania ni pazuri zaidi? Kama ulifikia hatua ya KUUKANA uraia wako na kujifunza tamaduni, sharia, historia tabia za mataifa mengine unatafuta nini Tanzania tena? Wadau walionitangulia wameliweka wazi vizuri. Njoo utembelee ndugu zako (mama yako, baba yako, wajomba, mashangazi, bibi yako, babu yako) uliowakana lakini tuachie sisi na u-bongo; U-Tanzania wetu. Tunajivunia kwa hilo kuwa mtanzania. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa. Huenda hata wimbo wa taifa wamesahau!

    ReplyDelete
  11. Asanteni Sana wanaDiaspora kwa ombi lenu.

    Sidhani mama Kuna mtu 'Aliyekana' uraia wake wa Tanzania kama wachangiaji wengine walivyoainisha. Na iwapo watakuwepo basi ni wachache. Na hawa wachache hawawakilishi wanaDiaspora wote.

    Nadhani neno zuri la kutumika hapa Ni 'Kupoteza' uraia baada ya kupata uraia wa nchi nyingine..

    Kuhusu uzalendo kwa nchi yetu tukufu Tanzania, naomba kuuliza Je yupi ni mzalendo zaidi yule anayeishi nje ya nchi/ughaibuni akifanya kazi halali na kujitahidi kutuma vijisenti kusaidia nyumbani au yule anayeishi Tanzania akifanya ufisadi na kunyonya rasili mali za nchi na kuhamishia mapato yake ya ufisadi nje ya nchi? Naomba pia ieleweke kuwa siyo kila mwenye uwezo wa kifedha ni fisadi. wapo wengi waliojipatia uwezo wa kifedha kwa njia halali.

    ReplyDelete
  12. Hoja hii imejaa walakini mwingi. Mfano, Diaspora wanasema kuwa kwao huko kunasaidia wao kuwa wanatuma vijisenti nyumbani--kwani hivi sasa hawatumi? Au nini tatizo?

    Hakuna binadamu duniani mwenye mama wawili, baba inawekana. Tunawezaje kupima uzalendo wa huyu 'ndumilakuwili' pale pande hizi mbili zinapoingia kwenye mgogoro.

    Bado nadhani utaratibu unaotumika hivi sasa hapa nchi unafaa zaidi na unaliondoa Taifa letu kujiondoa katika mtego wa 'matapeli'.

    Bwana Mangungu kuunga hoja mkono inatokana si na umuhimu wa hoja yenyewe bali washkaji alionao huko ughaibuni, lakini pia ukweli kwamba anamuunga mkono mwana Lindi mwenzake.

    Tafsiri ya neno raia kwa mara ya kwanza katika Tanzania imo katika Tamko la rais Nyerere kwenye mwaka 1961 wakati akitoa sifa za Mtanganyika. Alieleza kuwa raia wa Tanganyika ni wale wote waliozaliwa na kuwapo Tanganyika siku nchi inapata uhuru Disemba, 1961; pia wale wote wahindi kwa wazungu ambao watakuwa tayari kukana uraia wao na kuwa raia wa Tanganyika. Pia alieleza aina ya tatu ya uraia ni kwa watoto wote ambao walizaliwa na mmoja wa wazazi ambao si Watanganyika wakati huo--kwamba wakifikisha miaka 18 watakuwa na hiyari kuchagua wawe raia wa wapi.

    Uraia mwingine uliofafanuliwa ni ule wa kuomba kwa mujibu wa sheria. Uraia ulitafsiriwa ni mmoja tu--uraia wa Tanganyika. Ni waraka/hotuba hiyo iliyotumika kuunda sheria ya uraia ya Tanzania na nakumbuka hivi majuzi wakati ndugu Membe akihangaika kupigia debe hili alituma maofisa wake maeneo mbalimbali ili kupata hotuba hiyo ya Mwalimu Nyerere---imo kwenye kitabu Freedom and Unity.

    Msingi wa uraia wa uraia pacha hauwezi kuwa misaada na vijizawadi vya kutoka ughaibuni au ukarimu ambao walalaheri wetu huwa mnapata mnapotembelea huko. Tutafute kigezo kingine!

    Ahsante.

    ReplyDelete
  13. Uzalendo ni nini? Kipimo cha uzalendo nini? Kukaa ndani au ndani ya nje? Halafu hawa jamaa wanopinga uraia pacha mbona inakuwa kama mtu mmoja au wote wameenda shule moja!? Maana maneno yao na sababu zao ambazo hazina mantiki ni zile zile, kila wakitoa maoni humu? Halafu naona imekuwa fashioni siku hizi kuwasema jamaa wa Ughaibuni kama ilivyokuwa mtu akiwa na uwezo kidogo watu walimwiita fisadi. This people are the ones need to prove they're not robots, SMH.

    ReplyDelete
  14. Mdau wa 11 hapo juu:

    Haiwezekani kwa mtu mwenye akili timamu asiyekuwa Taahira kama unavyosema......''Nadhani neon zuri la kutumika hapa Ni 'Kupoteza' uraia baada ya kupata uraia wa nchi zingine''.......

    SASA MDAU KAMA WEWE NI MTU MZIMA NA AKILI ZAKO TIMAMU UTAPOTEZA VIPI KITU MUHIMU KAMA URAIA KIRAHISI NAMNA HIYO KAMA HUKUKUSUDIA ?

    NI WAZI BAADA YA KUUPATA URAIA WA NCHI ZINGINE MLIUDHARAU UTANZANI KAMA MLIVYOPELEKEA KUUPOTEZA NA SASA MNAONA UMUHIMU WAKE NDIO MNAZINDUKA USINGIZINI MNAUTAKA UTANZANIA!

    WAULIZENI WATU WA NCHI JIRANI ZAAFRIKA YA MASHARIKI ,Rwanda,Uganda, Kenya ,Burundi na Congo-DRC tuliwatimua mwaka jana kwa kunyemelea Ukazi wa kiholela haramua Tanzania.

    Hapa ndio mtaona umuhimu wa Utanzania upo wapi!!!

    Ninyi Madiaspora wengi kwa KUUPOTEZA URAIA kama unavyodai wewe ama WENGINE KUUKANA UTANZANIA na wengine kufikia hatua ngumu zaidi ya KUOMBA UKIMBIZI NJE YA TANZANIA hamfai kuaminiwa hata kidogo kupewa TENA Uraia wa Tanzania!

    Mmmetia aibu sana kwa kuwa mmeonekana ni Goigoi sana ktk suala la Uzalendo hivyo adhabu yake TUTAWAPA HATI ZA UKAZI WA KUDUMU NA SIO URAIA KAMILI mtakuwa mnaishi kama Wanaisrael Uhamishoni mkiwa kwenu Tanzania nchi ya asili yenu.

    ReplyDelete
  15. Ninyi Madiaspora sisi tulipo amua kuishi Bongo wakati wengine ulisha wahi kukaa Majuu huko mlituona Mafala!

    Sasa Mafala mmekuwa ninyi mliojiona Wajanja kwa kukaa Mamtoni!

    Ninyi si ndio mli punch kwa kuwa Majuu?

    Mnalia nini kuomba Uraia Pacha?

    ReplyDelete
  16. Madiaspora mnachekesha sana!

    Kama ingekuwa ni Idadi kubwa ya Pasipoti tungempatia Raisi wetu Jakaya Kikwete Tanzania No.1 !

    Sasa Mhe. Raisi Kikwete kipenzi chetu wananchi wa Tanzania anatumia Pasipoti moja (KWA KUWA NA URAIA WA NCHI MOJA) sasa tuwape ninyi Madiaspora muwe na Pasipoti mbili (2) si tututakuwa tumemdharau Mheshimiwa Raisi wetu JK?

    ReplyDelete
  17. Asante sana hapo juu,nakuunga mkono. Unajua wachangiaji wengi hapo juu wanaopinga jambo hili sound very short minded. No matter mtu kaamua kubaki nje baada ya kija kwa njia ipi,it's all about being able to help and support their families. Mbona watu Tz hapa wanalalamika kila siku kutokana naugumu wa hali ya maisha? wangapi wasomi hawana kazi? How much do the most earn? Watu wengine ni wivu tu unawasumbua, kama wangepata nafasi za kuondokea wengi wangeondoka kwenda kutafuta. Watu wanaoishi nje wanasaidia sana familia zao jamani, hiyo hiyo pesa wanayoituma inachangia kukuza uchumi wa nchi.
    Hivi Watanzania hamjui kuwa kuna nchi zinaproduce proffesionals Kwa ajili ya kuwa-export kwenda nchi za nje kufanya kazi?
    Kuna aliyezungumzia suala la uongozi, let me tell u, watu walioishi abroad have different thinking,mentality n.k. Exposure walionayo we do need it. Kwani mnafikiri nchi za wenzetu zinaendeshwa kama hizi zetu? those People have working systems. Watu hata maofisini mnafanya kazi kienyeji kienyeji tu, not responsible, mnaondoka mnapotaka, mnapiga umbea wakati mteja kasimama dirishani.

    Watanzania waishio nje wapewe tu opportunity ya kuwa na uraia wa nchi mbili,waweze kuja hata kufanya kazi tz wanapotaka, watasaidia hata kubadirisha hizi tabia mbovu za utz makazini.

    Hawa watu pia wana elimu nzuri sana, skills n.k. Bwana huko ukiwa kazini unajua ni nini unafanya, sio kazi za kuwekwa na mjomba.
    All in all Tz have a lot gain out of it.
    Guys don't be shallow minded.

    ReplyDelete
  18. Swali lilioulizwa hapo awali lilikuwa:
    Je mtu kuishi Tanzania ndiyo kipimo pekee cha uzalendo? Suala la utumaji 'vijisenti' lilitolewa kama mfano tu na wala siyo sababu kuu, wala ya msingi ya kuomba uraia pacha.

    Swali.
    Iwapo nchi nyingine wanachama wa East African Community wamepitisha uraia pacha, na iwapo raia wa EAC wanaruhisiwa kufanya kazi bila kibali nchini Tanzania jioni iwapo kazi itatangazwa hapa nyumbani Tz, Mkenya kwenye uraia pacha aishie ughaibuni ataweza tumia uraia wake wa Kenya kuja kupata/kufanya hiyo kazi kwa urahisi na yule Mtanzania halisia aishie ughaibuni atashindwa kwasababu sababu tu anauraia wa ughaibuni. Jioni kuwa hii inawapa COMPETITIVE ADVANTAGE ndugu zetu wa nch nyinginei za EAC?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...