Bunge Maalumu la Katiba limemchagua Mhe. Pandu Ameir Kificho (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba.
Katika uchaguzi wa nafasi hiyo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, Mh.Kificho ameshinda kwa Kura 393 sawa na Asilimia 69.
Washindani wengine, Bi.Magret na Mhe.Mahalu wamepata Kura 84 kila mmoja sawa na Asilimia 15.79%.
Akitangaza matokeo hayo Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah alisema Mhe. Kificho ameshinda baada ya kupata kura 393 sawa na 69.19% ya kura 558 zilizopigwa na kuwaacha kwa mbali washindani wake wa karibu, Mhe. Costa Mahalu na Mhe. Magdalena Rwebangira.
Awali Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila alitangaza kuwa Kuna Wagombea 4 wa nafasi ya Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, lakini katika hatua za Mwisho za Kujinadi kwa Wajumbe, mgombea Mmoja Mh.Sadifa (Mwenyekiti wa UVCCM na Mbunge kutoka Zanzibar)aliamua kujitoa kwa Kusema anamheshimu Mzee Kificho hivyo anaona ni vyema akamuachia.
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba ndiye atakayesimamia Kutunga Kanuni zitakazo tumika kwenye Bunge la Katiba. Mhe. Kificho pia ndiye Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar..
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...