Na Mwandishi Wetu
MIKOA sita imeomba kuandaa Tamasha la Pasaka mwaka huu.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka ndani ya Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka kumekuwa na maombi mengi sana ya wadau wanaotaka tamasha hilo.
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (pichani) alisema kwa sasa wanashughulikia vibali vya tamasha hilo na wala si vinginevyo.
“Yapo maombi mengi sana, lakini akili yetu kwa sasa ni suala la kupata kibali cha onesho lenyewe na baada ya hapo mambo mengine yatafuata.
“Sisi ni watu wa kufuata taratibu za nchi zinasemaje, ndiyo maana unaona hatuhangaiki sana kwa sasa na wanaoomba kuandaa tamasha, ila tukishapata kibali kutoka Basata (Baraza la Sanaa la Taifa), ndiyo mambo yatajipa zaidi,” alisema.
Kwa mujibu wa Msama, wadau wa muziki wa Injili wa mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Dodoma, Tanga, Dar es Salaam na Shinyanga ndiyo ambao mpaka sasa wameomba kufanyika tamasha hilo mikoani mwao.
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Krismasi kila mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...