MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.
Mdau Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo

MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.

Akizungumza kwa masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.

Anasema tukio hilo lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya kula na kufurahi na wenzake.

Anasema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.

Ameongeza kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.

Aidha kutokana na kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.

Amesema anahitaji zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri matibabu ya Mwanaye.

Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.


Na Mbeya yetu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. serikali inatumia mamilioni kwa siku kwa mambo ya kipuuzi kama katiba , huyu mtoto apelekwe na serikali india angalao akatibiwe , wanasiasa wao kwa chek up tu huenda afrika kusini, marekani , ujerumani na uingereza , mpelekeni huyu mtoto japo india acheni dhuluma , hizo pesa mtazozitoa ni zetu sisi walipa kodi

    ReplyDelete
  2. jamani malaika wa Mungu.....kwanini nchi isiwe inaangalia watu kama hawa sasa milioni mbili kwa serikali kusaidia mbona ni jambo dogo sana...rais wetu hupo wapi hapo kwa huyo malaika wa Mungu amenisikitisha sana ila ndio hivyo nami sipo vizuri kivile.Nchi za wengine zinavyojali watoto mbona angeishatibiwa mambo mengine yanakuja baadae.

    ReplyDelete
  3. Mwaisango, hongera sana kwa kutujuza habari hizi za kusikitisha. nafikiri Milioni 2 si kitu sema tu hata wengine tupo maskini lakini tungeweza kutoa tu. Mpigie simu au peleka ombi hilo kwa rais atamsaidia tu, kama aliweza kumsaidia Ray C atashindwa kwa malaika huyo? Tusiitupie sana lawama serikali wakati mwingine wanakuwa hawajapata hizo habari lakini nahisi wakizipata watashudhulika, kumbuka watoto mapacha waliopelekwa india kutenganishwa ni serikali ilifanya hilo kwa njia ya usitawi wa jamii.

    ReplyDelete
    Replies
    1. unajua kila kitu serekali inalaumiwa ingejuaje luna mtoto ana tatizo kama hilo. Huyo mganga alimtibu mara ya mwisho hakuona huyu mtoto anahitaji huduma ya kitalaamu zaidi akampa rufaa jamani? nina imani watoto hawahitaji bima ya matibabu. huyu mtoto atakuwa vizuri kabisa kama mkondo wa huduma ukifuatwa kpale hawpawezi apelekwe India au popote kama wanavyopelekwa wengine acheni ukiritimba mtoto ahudumiwe

      Delete
    2. kuna uzembe ulitendeka katika kumhudumia huyu mtoto hii hali ingezuilika kama wangechukua hatua ya kuhamishia huduma yake kwa watalaam. badoi hajachelewa ustawi wa jamii changamka huyu mtoto ahudumiwe. pengine mlikuwa hamjui vyombo vya habari vimeshaweka wazi kinachotakiwa hapa huduma na sio kusema raisi yuko wapi wahusika wawajibike au la wawajibishwe.

      Delete
  4. poleni sana kwa hili tatizo.

    ReplyDelete
  5. sikubaliani na mchangiaji wa tatu hapo anasema serikali haiwezi kulaumiwa , kwani huyu mtoto katoka nje ya nchi? aliungua nchi ya kigeni? jee hakutibiwa hospitali ya serikali mpaka akapona hayo makovu? muda wote hao wanaowakilisha serikali hawakumuona? acha kujipendekeza ndugu yangu kwa serikali rushwa , yule aliyepelekwa india kutenganishwa kulikuwa na namna kama kawaida na ulaji mkubwa umepita , fedha zilitumika kumtibu mtoto yule ni ndogo kuliko walizodai kuwa zimetumika kwenye bajeti zao, maofisa wetu serikalini hutumia shida za watu kujinufaisha ,

    ReplyDelete
  6. wachangiaji msilumbane nina imani wahusika wamesikia na wameona hali ya mtoto ombi letu ni mtoto kuhudumiwa. sidhani kama kuna mtu anajipendekexa hapa anajaribu kuondolea watanzania dhana potovu ya kulaumu badala ya kuchangia hoja in a constructive way. Ndio maana mwana blog anaonya usichafue hali ya hewa ktk uchangiaji. Jamani malaika ahudumiwe sio ajabu ni Makufuli wa kesho

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...