MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda wataalamu wamesema miongoni mwa mifumo ya fedha inayo kuwa kwa kasi hapa nchini ni VICOBA.

Alisema hayo alipokuwa akizindua rasmi muungano wa VICOBA wenye vikundi 46 na vikundi 25 vyenye jumla ya wanachama 600 ambao ndio waliopo katika mchakato wa muungano huo, Jana Mchana Jumamosi, Februari 15, 2014 katika Kata ya Kimanga Jijini Dar es Salaam.

Mfumo wa VICOBA umeendelea kushamiri na kuenea katika maeneno mbalimbali nchini ambapo wananchi wengi hasa wa kipato cha chini na asilimia kubwa wakiwa kina mama wameweza kunufaika na mfumo huu: “Inakadiriwa kuwa takriban asilimia 35 ya wananchi Kitaifa wanatumia huduma za fedha zisizo rasmi ambazo ni pamoja na VICOBA” alisema.

Mama Pinda aliongezea kuwa, taarifa hizi zinawapa faraja hasa kina Mama kwa kuona kuwa Serikali yetu inatambua Mfumo wa VICOBA na ambao umedhihirishwa kuwa wa Mafanikio makubwa.

“Ni matumaini kwamba Serikali yetu imejipanga vizuri kusaidia upatikanaji wa huduma za fedha kwa njia ya VICOBA kwa Watu wenye kipato cha chini na hasa Wakina Mama alifafanua Mama Pinda”.

Mama Pinda alisema, ninayo taarifa kwamba tayari Serikali yetu imekwishatoa maelekezo kwa kila Halmashauri kuhakikisha, Wanachama wa VICOBA wanapata mafunzo ya kuwapa uelewa wa dhana na Mfumo wa VICOBA ikiwa ni pamoja na jinsi vinavyoendeshwa na namna ya kujiendeleza: “Matarajio yangu ni kwamba maelekezo hayo ya Serikali yatawasaidia katika Vikundi vyenu mnavyovianzisha viwe na ubora zaidi na hatimaye kujikomboa katika umaskini wa kipato”alisisitiza.

Mama Pinda aliwashauri wana VICOBA kuangalia namna ya kuongeza hisa na michango kwa kila mwanachama ili kikundi kiweze kukua, kwani shilingi elfu 2000 kwa kununua hisa, shilingi 1000 kuchangia mfuko wa jamii na shilingi 500 kuendesha kikundi pamoja na shilingi 500 kwa ajili ya kumkopesha mwanakikundi endapo atakuwa na matatizo bado ni viwango vidogo kuendanda na hali halisi ya gharama za maisha na mahitaji.

“Natoa rai kwa wataalamu wa Benki, NSSF na Mifuko mingine wakishirikana na Serikali kutoa elimu ya VICOBA ili vikundi hivi viweze kujiimarisha” alisisitiza.

Miongoni mwa changamoto wanazokutana nazo wana vikundi hao wa VICOBA Kata ya Kimanga ni pamoja na uelewa mdogo wa wanavikundi kuhusu VICOBA na taasisi za fedha kudai riba kubwa kwenye mikopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...