Mshambuliaji machachari wa timu ya Yanga,Mrisho Ngassa (17) akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius wakati wa mtanange wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Dakika 90 za mchezo zimemalizika hivi punde na Yanga imeshinda kwa Bao 1-0 lililotiwa kimiani na Mrisho Ngassa,dakika ya 15 ya mchezo kipindi cha kwanza.
Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius akijiandaa kuondosha hatari iliyokuwa imekwenda langoni kwao.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga,Haroun Niyonzima pamoja na Beki wa Mbeya City,Yussuf Abdallah wakiwania mpira,wakati wa mchezo wao wa marudiano katika mzungunguko wa pili wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Mbeya City wakiendelea kuishangilia timu yao.
Mbuyu Twite wa Yanga akiangalia nani na kumpatia pasi wakati wa mtanange wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao la kwanza.
Msikate tamaa MBeya city, bao moja si kitu sana. Yanga ni timu ya muda mrefu sana kuliko ninyi. Hata hivyo mmejitahidi sana. Hongereni kaza mwendo.
ReplyDeleteKwa waamuzi hawa wa kibongo kazi ipo.
ReplyDeleteHatimaye Yanga yavunja mwiko wa Mbeya City!
ReplyDeleteHii ni Tambiko ya CCM kumimiza miaka 37 tena Maadhimisho yakifanyika hukohuko mjini kwenu Wanyampala wa Mbeya City!