Sophia Kindamba akiwa na mwanae Junior Richard Rutta .............................. |
MTOTO Junior Richard Rutta ambaye jinsia yake haieleweki anatafuta msaada utakaomuwezesha kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya CCBRT, jijini Dar es Salaam.
Mtoto huyo mwenye miaka miwili na miezi saba anaishi na mama yake mzazi, Sophia Kindamba, mtaa wa Mtwivilla, mjini Iringa.
Akiomba msaada huo, mama yake alisema jitihada za madaktari wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuchunguza na hatimaye kujua mtoto huyo ana jinsi gani zinaelekea kukwama.
“Kwa mara ya kwanza nilimpeleka katika hospitali hiyo mwanzoni mwa mwaka 2012, lakini hadi hii leo hakuna majibu yoyote; kwahiyo haieleweki kama ni msichana au ni mvulana” alisema huku machozi yakimtoka.
Alisema mapema mwaka huu alikwenda Muhimbili lakini kwa majibu aliyopewa amepoteza imani ya tatizo la mwanae kushughulikiwa hospitalini hapo.
Kindamba alisema “nimeambiwa kipimo kile kinatakiwa kupelekwa nje ya nchi baada ya uchunguzi wake hospitalini hapo kushindikana.”
Alisema wakati akipewa majibu hayo ameshauriwa akajaribu pia kupata vipimo hivyo katika hospitali ya CCBRT.
“Nimerudi Iringa kutafuta hela ili nikienda CCRBT nisipate shida ya gharama za uchunguzi na matibabu,” alisema.
Kindamba alisema Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa leo amempa barua itakayomuwezesha kupita kwa watu, taasisi na mashirika mbalimbali kuomba mchango.
“Naomba mnichangie; baba wa mtoto alinikimbi baada ya kubaini mtoto ana tatizo hili na sijui aliko; mimi mwenyewe nashindwa kufanya biashara yangu ya kutembeza mitumba kwasababu hali ya mtoto huyu sio nzuri,” alisema.
Alisema mtoto huyo huanguka na kupoteza fahamu kwasababu ana tatizo lingine la mtindio wa ubungo lililogundulika katika hospitali ya Muhimbili.
Iwapo umeguswa na upo tayari kumsaidia waweza kupiga namba0754026299 ili kuunganisha nguvu zetu.
Nina hakika hiyo itakuwa ni case ya Hermaphrodite ambapo mtoto anazaliwa na jinsia mbili ikiwa moja haijatengezeka vizuri (fully developed). Nafikiri suala ni kuangalia jinsia gani iko dominant na kuongezea hormones ili kuhakikisha jinsia moja inakuwa dominant. kwa mfano kama jinsia ya kiume ni prominent basi bora apewe tiba ya kuongezewa hormone ya kiume hii itasaidia kurekebisha tabia maumbile anapokuwa. kama ya kike ndio prominent basi itabidi apewe hormone ya kike ili kufanya mabadiliko stahili. Ila katika tiba zote mtoto hatoweza kuzaa kwasababu ya kutokuwa na ogani za uzazi zilizokuwa zimejengeka (lack of fully developed sex organs). Ila ataweza kuishi kama wengine bila ya kuwa na tabu kisaikolojia.
ReplyDeleteHermaphrodte sio ajabu hutokea japo ni nadra kutokea.
The mdudu,sivizuri kutumia neno mtt wa ajabu,nadhani ingekua vyema kama mngeandika mtt mwenye matatizo coz huyu mtt ni mwanaadam sio mnyama.pole sn mm mweye mtt tupo pamoja nimeiona number ntajitahidi nitume nilicho nacho coz inasikitisha sn kuona baazi ya MIJUMBE Inadai kuongezewa MIPOSHO huku wakijua fika kuna watanzania wenye shida kama hawa akina MAMA ZETU lo washindwe wao na walegee kama bamia.
ReplyDeleteKila mjumbe wa BUNGE LA KATIBA,anaweza kuchanga elfu moja tu katika ile posho yao.
ReplyDeleteKwanjia hii mtarudisha imani kwetu.
mie sijamuelewa huyo katibu tawala kumpa barua ya kuzunguka kuomba hela.
ReplyDeletehivi tanzania hatuna huduma za jamii, afya na matibabu?
nyie diaspora mnaotundika sura zenu kwa michuzi blog, mbona hampiganii mambo kama haya?
wanasiasa hao wana yao ya 2015, kwahiyo wanajali zaidi umaarufu kuliko mustakabali wa nchi yetu baada ya 2015.
Huyu si mtoto wa ajabu hii inaitwa Hermaphrodite kwa lugha ya kitaaluma. Inatakiwa aangaliwe na kujua jinsia gani ina nguvu na apewe hormone kuongezea nguvu kwenye hiyo jinsia, basi hakuna shida yeyote. Mkimbiaji mmoja wa Afrika ya Kusini yupo hivi na walikuwa wanadhani ni mwanaume.
ReplyDeleteDr. L. Pim, Kibada.
Kwa kutumia Saikolojia yangu kwa kumtazama ktk picha motto anaonekana ni DUME!
ReplyDeleteNi vile tu labda kwa kuwa hana hicho kiungo.
Hahahahahaha!
ReplyDeleteMdau wa 3 hapo juu, naungana na wewe, yaani sisi tunahangaika buree wakati Mabosi wa Mapesa tunayo hitaji kwa shida iliyopo mbele yetu wapo Dodoma kwenye Bunge la Katiba tena wakizidi kuomba waongezewe mafao!
Tutawapitishia nao Bakuli!