TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO
VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 01.02. 2014.
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA KATIKA
AJALI YA BARABARANI.
gari ambalo halikuweza kufahamika namba zake za usajili wala jina la
dereva wake lilimgonga mtembea kwa miguu mwanafunzi wa darasa la pili katika
shule ya msingi mbuyuni aliyetambulika kwa jina la daima faida (08) mkazi wa mbuyuni na kusababisha kifo chake papo
hapo. ajali hiyo ilitokea majira ya saa 06:55hrs
asubuhi wilayani mbarali mkoa wa mbeya. chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi, dereva alikimbia mara baada
ya tukio. mwili wa marehemu umekabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi. juhudi za
kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea. kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina
msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. msangi anatoa wito kwa yeyote mwenye
taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio hili azitoe katika mamlaka husika
ili akamatwe na sheria ichukue mkondo wake.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...