George Masaju (pichani) amedai mahakamani katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba kwa mujibu wa katiba mamlaka ya mahakama kuingilia mwenendo wa bunge yameondolewa.
Pia, Mhe Masaju amedai kuwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi bunge halina mamlaka ya kuingilia mwenendo wa mahakama na kwamba kesi iliyopo mahakamani haina mashiko ya kisheria mahakama itupilie mbali.
Kesi hiyo ya Kikatiba inasikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu, likiongozwa na Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, akisaidiana na Jaji Augustine Mwarija na Dk. Fauz Twaib.
Mhe. Masaju alitoa madai hayo jana wakati akijibu hoja za upande wa walalamikaji kwamba kesi iliyopo mahakamani ina mashiko ya kisheria.
“Watukufu majaji, kwa mujibu wa kifungu cha 4 kidogo cha 4 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinaeleza kwamba kila chombo kitaundwa na kutekeleza majukumu yake… mahakama haina mamlaka ya kuingilia mwenendo unaotokea bungeni na kwa utaratibu huo, wabunge wanazuiliwa kujadili masuala yaliyoko mahakamani” alidai Mhe Masaju.
Mbali na Mhe Masaju upande wa walalamikiwa, mawakili wengine ni, Mawakili wa Serikali Wakuu, Gabriel Marata, Sara Mlipano na Alesia Mbuya.
Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa kesho ambapo upande wa walalamikiwa watato hoja zao.
Katika madai ya msingi LHRC na TLS waliwasilisha madai mahakamani wakidai wanapinga kauli iliyotolewa na Mhe. Pinda bungeni, Juni 20, mwaka huu, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo.
Mhe.Pinda anadaiwa kutoa kauli inayolalamikiwa alipokuwa akijibu swali la
nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu
aliyetaka kujua msimamo wa serikali na mambo mengine, malalamiko dhidi
ya vyombo vya dola katika baadhi ya maeneo kama Mtwara, kuwapiga
wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...