Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala mwishoni mwa wiki aliendelea na ziara ya siku tano ya kuangalia miradi ya maji jijini Dar es Salaam na Pwani, ambako alifika Kimbiji na Mpera kuangalia mradi wa visima virefu vya maji.
Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa akimuonyesha Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala ramani na mpango wa uchimbaji wa visima vya Kimbiji na Mpera.
Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa akimuonyesha Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala kisima cha Mpera.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala akisikiliza maelezo kutoka kwa Inj. Romanus Mwang’ingo wa DAWASA (kushoto ktikati) katika kisima cha Kimbiji na Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa (katikati) akisikiliza.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala akifungua maji katika mradi kisima cha Kimbiji, akiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kichangani, Mbegu Miraji.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala akisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkandarasi kuhusu kisima cha Kimbiji.
Mradi wa maji wa kisima cha Kimbiji chenye mita 600 kikiwa katika mchakato wa kuchimbwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...