Na Hellen kwavava

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali ya wadau wa elimu kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 21 mwaka huu ambayo ni viwango vya ufaulu, alama ya chini ya ufaulu na ufaulu wa jumla wa mtahiniwa.

Akitoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza hilo Dakta CHARLES MSONDE amesema viwango vya ufaulu ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na wale walio katika kundi jingine.

Amesema mkanganyiko uliojitokeza katika mitihani hiyo ni kutokana na baraza kuanza kutumia utaratibu wa makundi 7 ambayo ni A ikiwa ni 75-100,B+ ikiwa ni 60- 74, B ikiwa ni 50-59, C ikiwa ni 40-49, D ni 30-39, E ni 20-29 na F ni 0-19 lengo likiwa ni kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja.

Ameongeza kuwa madaraja hayo yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)6 cha kanuni za mitihani ambacho kinaeleza kuwa ufaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama na ufaulu katika daraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu katika masomo yasiyopungua mawili.

Kuhusu kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja MSONDE amesema ufafanuzi utatolewa na Kamishna wa elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tulizoea kuwa ili mtu aweze kufanya mtihani wa Form Six,lazima awe na credits tatu (C na kuendelea). Je, bado sharti hili liko pale pale?? Au sasa ni B na kuendea?

    ReplyDelete
  2. uzuri c imebaki ni 40+ na shule nyingi hupenda hiyo iwe minimum.

    ReplyDelete
  3. La muhimu nikuboresha elimu, ili matokeo ya juhudi za wadau wote kuhakikisha kuwa wanaosoma wanaelewa, matokeo mazuri tuanze kuyaona miaka ya karibuni.

    ReplyDelete
  4. je kwa wale wanao rudia (resit) unakuta mtu alikua ana D tatu sasa akaamua kurudia somo moja au mawili somo moja akapata D' kwa jumla na zile tatu ni nne je anaweza kujiunga na chuo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...