Wafuasi wa CCM Iringa wakimpongeza kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kwa kufanikisha chama hicho kushinda uchaguzi mdogo kata ya Nduli.
Wafuasi wa CCM kata ya Nduli wakiwa wamemnyanya juu juu aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Nduli Bw Mtove baada ya matokeo kumpa ushindi wa kishindo leo
...........................
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimefanikiwa kutetea kata zake zote tatu ambazo leo wananchi wameshiriki kupiga kura kuwachagua madiwani kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki dunia.
Wafuasia wa CCM walimpongeza aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga na kudai kuwa kazi yake inaonesha wazi safari yake ya kulitwaa jimbo la Iringa mjini.
Matokeo katika vituo vyote tisa ambavyo wananchi wa Nduli walipata kuvitumia kupiga kura ,kituo cha Mawasiliano CCM (57),Chadema(28),Zahanati CCM( 114), Chadema ( 47), Shule Nduli CCM(70) Chadema(39), KIngonzile shule CCM(105) Chadema(82),Mibata CCM(48) Chadema(103), MTalagala CCM(95),Chadema(54),Godauni CCM(138 ,Chadema(52),Njiapanda CCM (75) Chadema (52),Msisina CCM (156 ) Chadema (31)
Katika Matokeo hayo ambayo hadi sasa majira ya saa 12.50 bado msimamizi wa uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 854 huku Chadema wakifuatia kwa kura 487
Mbali ya matokeo hayo ya kata ya Nduli pia CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za wilaya ya Kilolo.
Katika kata ya Njombe mjini mgombea wa Chadema amembwaga mgombea wa CCM ambapo matokeo yanaonyesha mpinzani wake ameongoza katika kituo kimoja pekee kwa tofauti ya kura 2 huku katika vituo vyote Chadema ikiibuka kidedea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...