Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmuod Thabit Kombo, akizungumza na Waandishi wa habari na kutowa shukrani kwa wapinga kura wake na WanaCCM waliomuunga mkono katika safari ya Kampeni na kuahidi kutimiza ahadi zote alizoahidi kwa Wananchi wa Jimbola Kiembesamaki na kuondo kero zote na kuwaletea maendeleo katika jimbo lao.
---------------------------------------------
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameibuka Kidedea kwa ushindi alioupata katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo baada ya kukaa wazi kwa muda mrefu kutokana na kutenguliwa kwa aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.
  Akitangaza matokea hayo ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki yalioshirikisha Vyama Sita vya Siasa vilivyosimamisha wagombea wake. Msimamizi wa Uchaguzi Ndg. Suluhu akitoa matokeo hayo Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameshinda kwa Kura 1856, sawa na asilimia 75.1 na kutangazwa mshindi wa Uchanguzi huo Mdogo wa jimbo hilo kuchukuwa nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Mansoor Yussuf Himid, aliyevuliwa Uwanachama na CCM na nafasi hiyo kuwa wazi kwa muda hadi kufanyika kwa uchaguzi mdogo leo na kumpata mrithi wa kiti hicho. 
 Mgombea wa Chama cha CUF Mhe. Abdulmalik Juma Jecha, amepata kura 445, sawa na asilimia 18.3, Mgombea wa Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid amepata kura 84, sawa na asilimia 3.5, Chama hichi ni kipya kimeungwa na Viongozi walioondoka CUF, na hii ni mara ya pili kushiriki Uchanguza tangu kuanzishwa. Kilishiriki uchaguzi wa kwanza kisiwani Pemba katika jimbo la Chambani,Pemba. 
 Nae Mgombea wa Chama cha CHADEMA Mhe. Hashim Juma Issa,amepata kura 34 sawa na asilimia 1.5, katika uchaguzi huo mdogo wa jimbo la kiembesamaki.Mgombea wa TADEA Ali Mohammed Ali (Mbongo) amepata kura 6 sawa na asilimia 0.3. wakati Mgombea wa Chama cha SAU Mhe. Ramadhani Simai Mwita amepata kura 1 sawa na asilimia 0.1 
 Kwa matokeo hayo Tume ya Uchaguzi Zanzibar imemtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki na anakuwa Mwakilishi halali baada ya ushindi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. CCM juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu X TRILLIONI ZOTE!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Kamanda. Ninajua uwezo wako. Ni matumaini yangu watu wa jimbo la Kiembesamaki wamelamba dume na watafurahia uwakilishi wako. Kila la kheri kwenye majukumu yako mapya. Mungu akuongoze. Amina.

    ReplyDelete
  3. mm nilijua mapema mahmud atashinda kwa sababu hawasomi alama za nyakati kwa mara nyingine cuf wanasimamisha mgombea ambaye hauziki kwa siasa za sasa hivi ili ushinde usimamishe mgombea ambaye ni maarufu kwa watu mwenye uwezo na anayejiamini

    ReplyDelete
  4. chadema imepitwa na ADC? Lo, aibu hiyo. 1.5% si wajiachie kuingilia siasa za Zanzibar? Hawaziwezi

    ReplyDelete
  5. Yu wapi babu silaaaaaaa, halafu chadema wanajigamba kuchukua nchi, thubutuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...