ABIRIA mmoja kati ya 28 amekufa papo hapo na wengine kulazwa Hospitali
ya mkoa wa Lindi, Sokine,kufuatia basi la kampuni ya CHALA Express
walilokuwa wakisafiria kutoka Jijini Dar es salaam kwenda wilaya ya
Newala mkoani Mtwara, kukwaruzana na Lori.
Abiria aliyepoteza maisha katika ajali hiyo anaitwa Amina Omari
Makodora (48) mkazi wa kijiji cha Kilindoni,wilaya ya Mafia,mkoani
Pwani.
Kwa mujibu wa abiria wengine walionusulika kwenye ajali hiyo,wameiambia Globu ya Jamii kuwa ajali
hiyo imetokea eneo la kijiji cha Kilangara,kilichopo katika
Halmashauri ya wilaya ya Lindi,saa 8:0 mchana.
Abiria hao waliokuwa wakisafiri na basi hilo la kampuni ya Chala
Express namba T. 699 ATK linaloendeshwa na dereva,Haji Chande Chondo
(56) mkazi wa Jijini dar es salaam,linalofanya safari zake kati ya
Jiji na Newala.
Dereva Chondo ameliambia gazeti hili Hospitalini hapo kuwa, wakati
akiwa katika eneo hilo aliweza kukutana na Lori lililokuwa limebeba
kijiko kutoka mikoa ya kusini na kuelekea wilayani Kilwa.
"Hili Lori lilikuwa linatelemka mlimani na mimi pia,hivyo mwenzangu
akaniwashia taa na kunifanya nipunguze mwendo na kubana zaidi
kushoto"Alisema Chondo.
Chondo alieleza kuwa wakati akiwa amejaribu kubana pembeni zaidi ndipo
Lori hilo ambalo bado namba zake hazijaweza kufahamika mara moja,
likamkwaruza sehemu ya ubavu wa kulia wa basi na kusababisha kifo cha
mmoja wa Abiria wake na wengine kuumia sehemu mbalimbali ya miili yao.
Alisema mara baada ya kumkwaruza Lori hilo halikuweza hata kusimama
badala yake aliendelea na safari yake bila kujali nini kimetokea au
usalama wao.
Hatibu Nassoro mmoja wa abiria wa basi hilo, amesema kama gari yao
ingekuwa katika mwendo mkali,lingeweza kupinduka na kusababisha maafa
makubwa.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dkt, Muhaji Mohamedi amekili kupokea
mwili wa marehemu Amina Omari Makodora,wakiwemo na majeruhi tisa (9)
waliokuwa wakisafiri na basi hilo,huku mmoja akiwa bado hajaweza
kutambuliwa mara moja.
Amewataja majeuhi hao kuwa ni,Asha Mohamedi Buriani (43),Zuhura
Maulidi (28) mwenyeji wa Tandahimba,aliyeumia kichwani,Hadija Chiwaya
(36),Asha Mohamedi (43) haji Chondo (56) ambaye pia ni dereva wa basi
hilo.
Wengine ni Rashid Mchowanje (60) aliyeumia bega la mkono wa kulia na
Anifa Mwenye (17) mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari
Kiregezi kata ya Mkunya,wilaya ya Newala aliyepata michubuko mkono wa
kulia na mwingine ambaye jina lake bado halijaweza kufahamika mara
moja.
Dkt Muhaji amesema majeruhi watatu kati ya hao wamelazwa Hospitali
wakiendelea na matibabu ambapo wengine sita wametibiwa na kuruhusiwa
kuendelea na safari zao.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoani Lindi,Joseph Mfungomara amekili kutokea
kwa ajaili hiyo, na kueleza kuwa basi hilo lilikuwa na abiria 28,na
kwamba Jeshi hilo linaendelea kumsaka dereva wa Loli aliyesababisha
ajali na mauwaji wa abiria huyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...