Watu 12 rais wa Iran na Pakistani wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, wakikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na kuingiza nchini kilo 200.5 za dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya Sh. bilioni 9.022. 
 Washtakiwa hao ni, Kepteni Ayoub Mohamed raia wa Irani, Wavuvi, Buksh Mohamed raia wa Pakistani, wa Irani Buksh Mohamed, Fahiz Dauda, Rahim Baksh wa Pakistani, wa Iran Khalid Ally na Abdul Somad. 
Wengine ni raia wa Pakistani Abdul Bakashi, wa Iran Saeed Sahury, Bashir Afraz, Morad Gwaram na Hazir Azad. 
Washtakiwa hao walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba wa mahakama hiyo. 
 Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Prosper Mwangamila, ulidai kuwa Februari 4, mwaka huu washtakiwa wote walikutwa ndani ya bahari ya Tanzania wakiingiza dawa za kulevya aina ya heroin nchini. 
 Ilidaiwa kuwa dawa hizo ni kilo 200.5 zenye thamani ya Sh. 9,022,500,000 aina ya heroin. Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. 
 Hakimu Mwaseba alisema kesi hiyo itatajwa Februari 24, mwaka huu na washtakiwa wapelekwe mahabusu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Bro Michuzi, CNN wameonyesha leo hii news na wamesema ni coast guard wa Australia ndio waliokamata na sio polisi wa bongo. Sasa hii imakaaje.

    ReplyDelete
  2. Raia sio 'rais'! Editing, editing, editing!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...