Kama ulikuwa haufahamu, habari kuu katika ulimwengu wa Teknohama kwa siku ya leo ni Facebook kuinunua Whatsapp kwa bei ya dola bilioni 19.  
Nunuzi hilo ni la programu pekee na siyo kampuni ingawa wafanyakazi wa whatsapp watajiunga na timu ya Facebook moja kwa moja, mission za whatsapp zitaendelea kubaki kama zilivyo, alieleza Jan Koum ambaye ni muanzilishi wa whatsapp.

Kwa wasio fahamu, whatsapp ni moja ya programu ya simu za mkononi inayokuwezesha kutuma ujumbe wa simu kupitia kwenye intaneti badala ya ujumbe mfupi (sms). Kwa kutumia whatsapp, inamaana utaepuka gharama za sms huku ikiwa imesheheni matumizi mengine mengi zaidi kama kutuma picha, sauti uliyojirekodi nk.

Hadi sasa, whatsapp ina watumiaji hai milioni 450 kila mwezi kutoka nchi nyingi duniani, huku kukiwa na watumiaji wapya zaidi ya milioni moja kila siku. Hivyo, ni dhahiri kuwa whatsapp ni programu pendwa na yenye kutumika.

Whatsapp inaweza kutumika kama njia rahisi zaidi ya mawasiliano kwa watu binafsi na hata makampuni, kwa mfano, sisi Dudumizi tunatumia whatsapp kama njia ya kuwasiliana na mamia ya wateja wetu walio nje ya nchi na kutuwezesha kupunguza gharama za mwasiliano.

Ingawa makampuni mengi ikiwemo Facebook yamekuwa yakitegemea huduma za matangazo kama njia ya kuingeza kipato, whatsapp ni programu ambayo, huwezi kuonana na matanagazo na wamejizatiti kuwa ni wataendelea hivyohivyo bila ya matangazo. Na pia whatsapp ni bure kwa kwa mwaka wa kwanza na huchaji $1 kwa mwaka kama gharama ya kujiunga kwa miaka inayofuata. Hivyo kabla ya Facbook kuinunua whatsapp ni dhahiri walishajipanga kwenye hili, kwani, hili ndilo linaloifanya whatsapp iwe tofauti.

Akielezea sababu ya kuinunua whatsapp, mwanzilishi wa Facebook alisema, wameinunua whatsapp kwa sababu whatsapp ina thamani. Na wao wakiwa kama wafanya biashara lengo lao kubwa ni kuongeza thamani ya biashara yao illi waendelee kuwa salama. 
Hivyo, wanaamini nunuzi la whatsapp litakuwa na tija na manufaa kwa wote, wanunuzi na walionunuliwa. Hivyo ubora na misingi ya huduma ya whatsapp utaendelea kuwa juu kama ilivyo sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tegemea Matangazo Ya Biashara Kwa sanaaaaaaaaaaaaaa

    Kila Ukituma Ujumbe wenye Neno Kama
    "Bia" Utapata Message inakuonyesha Baa za Karibu na Bia Mbalimbali

    ReplyDelete
  2. Eti FB ni mali ya Freemason?. Eti wamenunua Whatsapp kuunganisha na kupata data zetu zote?


    ReplyDelete
  3. Hapo tegemea kupiga simu kwa Mitandao ya bei ya juu wa Bongo badala ya 'meseji za simu za picha' za bure ulizotumia kwa muda mrefu sasa!

    Na sasa Mabepari wamesha uziana mchongo.

    Hujui ya kuwa cha mwenzako sio chako?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...