Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua
 Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii
 Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii

 Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
 Hii ni njia ya mlima sekenke
Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida na kuua watu wanne hapohapo.
Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.
Shuhuda wa ajali hiyo bwana Julius chacha alipoongea na mtandao wetu wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.
Watu wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali hiyo. Polisi walikuwa bado hawajafika eneo la tukio mpaka tunaondoka eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wot is next? Jee Watanzania mnahisi kifuatie kipi kuepukana na vilio kama hivi?

    ReplyDelete
  2. Pôle kwa wote waliofikwa na msiba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...