Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombelezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72)  aliyefariki  dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI)  jijini Dar es Salaam.

Marehemu Qorro ambaye wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwamo Waziri mdogo wa Kilimo na Ushirika na baadaye kuwa waziri kamili wakati wa awamu ya pili, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvuja damu kwenye mzunguko wa kichwa kulikosababishwa na hitilafu ya figo.Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. James Bwana, Marehemu anatarajiwa kuagwa rasmi kesho kabla ya kusafirishwa Jumatano hadi Kijiji cha Mbulumbulu, wilayani Karatu, mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Dkt Martha Qorro na wanafamilia wengine nyumbani kwa  aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72)  aliyefariki  dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI)  jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni familia kwa kipindi Niki kigumu Mungu awatie nguvu na kuwapa faraja,maana no mwezi wa kumi na mbili Dr grace Qorro alimpoteza mumewe na sasa baba. So msiba was familia tu ni wa taifa zima aliwasaidia wengi bila kuchagua mtu,mpenda haki,jirani mwema nk.tumwenzi kwa Yale aliyotushauri kuyafanya na kuiga mfano wake,ni mfano wa kuigwa.poleni familia,ndugu na marafiki,na kwa wale wanaodhamini mchango wake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...