Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa India Mohamed Hamid Ansari wakati walipokuwatana nchini India.

Tanzania na India zimeeleza kuridhishwa na uhusiano na ushirikiano uliopo baina yao na kusisitiza dhamira ya kweli ya kuona kuwa ushirikiano huo unazidi kuimarika kwa manufaa ya Serikali na wananchi wa nchi hizo.

Hayo yamejitokeza leo wakati wa mazungumzo kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa India Mohamed Hamid Ansari.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamesema kuwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo ulioanzishwa mwanzoni mwa miaka ya sitini umekuwa ukiimarika mwaka hadi mwaka kwa kuongeza maeneo ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali za uchumi na kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jeez what is Makamo uandishi siku hizi umekuwaje nachukia sana wanao haribu Kiswahili na hakuna anayeonekana kujali. Halafu tunataka kuwafundisha watu wengine Kiswahili, kipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...