Mwenyekiti wa maandalizi ya Kongamano la Viongozi wa Dini mikoa ya Lindi na Mtwara MohamedSenani akiwakaribisha wajumbe katika kongamano la viongozi hao katika ukumbi wa VETA mjini Mtwara. Kongamano ambalo viongozi hao walijadiliana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizungumza na viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa kongamano la viongozi hao lililohusu rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madinikwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Baadhi ya wajumbe wa kongamano la viongozi wa dini wakiwasili eneo la Mnazi Bay kujionea shughuli za namna visima vya gesi vinavyofanya kazi na kuzalisha gesi ambayo ni moja ya chanzo cha nishati ya umeme kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu.
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
Ankal, wasalaam aleikhum. nimefurahishwa na picha ya uliyoitundika hapa ambapo kiongozi wa dini ya kiislam na wa dini ya kikristo wameshikana mikono wakijadili jambo flani. picha hii inaonyesha jinsi ambavyo watanzania tunavyopendana bila kujali itikadi zetu za kidini. ni picha nzuri kuwahamasisha wantanzania wote ili tupate kuishi kwa upendo na mshikamano kama viongozi wetu wafanyavyo. napendekeza picha hii uikuze na ikiwezekana itumike katika kuhamasisha masuala ya kujenga ushirikiano na amani Tanzania.
ReplyDelete