Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akiwaongoza Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania katika Maandamano ya kuadhimisha Siku ya Sheria nchini leo asubuhi katika viwanja vipya vya Mahakama vilivyopo Mtaa wa Chimala karibu na Southern Sun Hotel.
   Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika Sherehe za Siku ya Sheria nchini.
      Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Augustine Ramadhan  akiwa pamoja na Viongozi wengine wastaafu wa Mahakama katika sherehe hizo zilizofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman mara alipowasili katika viwanja hivyo kama Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo.

 Ukaguzi wa gwaride kuashiria uzinduzi rasmi wa Shughuli za Mahakama kwa mwaka 2014
   Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa na Majaji wenzake wakipokea heshima ya gwaride katika sherehe hizo katka viwanja vya Botanical Ocean road jijini Dar es salaam leo asubuhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. kama maaskofu! lol

    ReplyDelete
  2. Great but I don't see this (siku ya sheria duniani) on International Days calendar (UN).

    ReplyDelete
  3. Hicho kiubao na kiji-carpet uchwara alichosimama Jaji mkuu vinaitia aibu nchi. Jamani nchi nzima imeshindwa kuandaa kigoda bora au ni ile attitude ya "don't care" bora liende. Tuwe conscious jamani siku hizi tujitahidi kuwa nadhifu and creative kwani news zinasambaa mbali na haraka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...