Asia Idarous akipita kwenye red Carpet
Asia Idarous akipita kwenye red carpet

MAMA wa Mitindo nchini na Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin amewashukuru wadau mbali mbali kwa kuendelea kuliunga mkono onesho la Mitindo la kila mwaka la 'Lady in Red' ambalo kwa mwaka huu limetimiza miaka 10 tokea kuanzishwa kwake huku likiwa la mafanikio kwa kuibua wanamitindo wakubwa hapa nchini.

Akizungumza Dar es salaam, katika ofisi za Fabak zilizopo Msasani jirani na Kwa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, Asia Idarous alishukuru wadau mbali mbali waliojitokeza siku hiyo sambamba na wadhamini waliofanikisha kwa shughuli hiyo kubwa hapa nchini.

Asia alisema ni jambo la fadhira kwa kushukuru huku akiahidi kuboresha kama kulikuwa na mapungufu ya hapa na pale. 
"Muungwana ni vitendo, ‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’ ilikuwa ni ya kipekee kwa mwaka huu, hivyo nawashukuru nyote kwa kuliunga mkono jukwaa la Lady in red 2014, kwa kutimiza miaka hii 10" alisema Asia Idarous.

Aliongeza kuwa, kuelekea onyesho la mwakani kwa mwaka 2015, jukwaa hilo la Lady in Red, linatarajia kuwa la kimataifa ikiwemo wabunifu wa kimataifa kuonyesha ubunifu wao hapa nchini.

"Kwa sasa tunaelekea anga za kimataifa kupitia jukwaa hili hili la Lady in red, zaidi ni kuendelea kuliunga mkono ilikutimiza ndoto hizi, na hii itasaidia kufungua milango ya wabunifu wetu kujiuza nje ya mipaka yetu" alisema Asia Idarous. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...