![]() |
Mashabiki wa Simba |
Matokeo ya mchezo la ligi kuu ya Voda Com si Simba wala Mbeya City baada ya timu hizo zote mbili kutoka uwanjani hapo kwa kifua mbele cha goli 1-1.
Mchezo huo ambao kwa Mbeya City ni mchezo wa nyumbani imeweza kuonyesha umakini mkubwa wa kugomea kufungwa katika uwanja wa Nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya huku Simba nayo ikikwepa " kugagaduliwa " ugenini kiasi cha kuifanya Simba kukomaa na kusawazisha goli la Mbeya City lililofungwa kipindi cha kwanza huku Simba ikisawazisha goli hilo kipindi cha pili.
Timu ya Mbeya City ambayo awali iliweza kufanya vema kwa Yanga kulazimisha sare pia leo imeweza kulazimishwa na Simba kutoa sare ya goli 1-1.
Wakati huo huo timu ya Lipuli Fc Iringa imefanikiwa kuichapa timu ya Polisi Morogoro katika mchezo wa ligi daraja la kwanza mzunguko wa pili kwa jumla ya goli 3-1.
Mchezo huo umechezwa katika uwanja wa Samora mjini Iringa huku wadau wa soko wakiipongeza kwa mchezo huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...