
Sanya Juu ni mji mdogo ndani ya wilaya Siha Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni Km 25 toka Bomang'ombe na KM 50 toka Moshi Mjini, weekend hii nilifanikiwa kuutembelea Mji wa Sanya Juu ambapo siku ya Jumamosi mji huu huwa umechangamka kwa shamrashamra za kibiashara. katika pita pita zangu nilifanikiwa kulitembelea soko la mji huo, ila nilishangazwa na hali niliyo ikuta ya miundombinu isiyo kidhi na kulifanya soko kuonekana hatarishi kwawafanya biashara na wateja wao kiafya.
Huu ni msimu wa mvua kwa sehemu kubwa ya mkoa wa Kilimanjaro, hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa kuimarisha miundombinu ya soko la Sanya Juu kuimarisha afya za wafanyabiashara na wateja wao.


hali hii pia ni kero kwa watembea kwa miguuu sokoni hapo.

Msimu huu wa mvua unasababisha kero hii kwa baadhi ya wateja hata wafanyabiashara sokoni.


Baadhi ya wachuuzi wakiwa sokoni hapo kununua mahitaji yao lakini mazingira ya soko hayaridhishi kutokana na uchafu uliokithiri hapo na kuhatatrisha afya za walaji wa bidhaa

Hii ni njia ya kuelekea soko hili ikiwa imejaa matope kutokana na kuwa katika kiwango cha changarawe.
Picha zote na mdau Wito Msafiri wa Mwanaharakati Mzalendo Blog.
Hii hali ya matope na kukosa mpangilio unaoeleweka ikiwa ni pamoja na miundo mbinu ya maana sokoni haifai kabisa. Wanaohusika watumie ushuru na vyanzo vingine kujenga soko la kisasa.
ReplyDeleteUshuru unafanya nini? Reflection ya kasi mpya na ari mpya. Uchaguzi 2015 changua kiongozi atakayefanya mabadiliko. mkuu wa sijui wilaya atakuwa hajaliona hili?
ReplyDeleteOk, hivi waAfrika/waTanzania tutaamka lini. Kama kila siku mnasubiri mtu aje awafanyie, mtasubiri kweli. Hivyo hao wafanyabiashara wote hapo sokoni wanashindwa kujipanga na kwenda kutafuta mchanga au kokote na kuja kuweka kwenye hayo matope ili wafanye biashara sehemu iliyo salama. Halafu, ikifika wakati wa uchaguzi wakumbusheni hao mnaowachagua kwamba sie hatukuchagua tena, ulikula hela yetu ya ushuru ukashindwa hata kututengezea soko letu, tumetengeneza wenyewe. Taifa letu litajengwa na sie wenyewe. Nyie kaeni tuu msubiri mtu aje afanye...mtasubiri kweli.
ReplyDeleteUkisema utaambiwa mchochezi, sijui ni watu gani hawa wasiotaka kukosolewa.....
ReplyDeleteDu! Wenyeji na wafanyabiashara washirikiane kutengeneza hilo soko kwani ni lao wote. Ushuru unaotozwa utumike kununulia mchanga/kokoto na nguvu za wanachi zisaidie kutengeneza. Tuelewe kwamba serikali ni mimi na wewe.
ReplyDelete