Siku ya Jumamosi tarehe 22 Februari 2014 kilifanyika kikao baina ya Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe pamoja na wawakilishi wa Watanzania kutoka vitongoji vya London na maeneo mengine nchini Uingereza.Kikao hicho kilijadili haja ya kuandaa Mkutano wa Diaspora nchini Uingereza mwaka huu 2014. 
Katika majadiliano ilisisitizwa umuhimu wa kuwa na mikutano ya Diaspora hasa kwa malengo makuu yafuatayo: 
• Kuwaleta karibu watanzania waishio maeneo mbalimbali nchini Uingereza. 
• Kuwaweka karibu Watanzania na Serikali yao
 • Kuwatangazia Watanzania fursa zilizopo nyumbani katika sekta za maendeleo. 
Baada ya majadiliano kikao kiliona haja ya kuandaa kamati ya muda (Tanzania UK Diaspora Task Force) itakayosimamia mchakato wa maandalizi ya Mkutano wa Diaspora mwaka huu 2014. Kamati hiyo itakuwa chini ya Uenyekiti wa Bi Mariam Kilumanga akisaidiwa na Bw. Cleopa John katika nafasi ya Katibu. 
Aidha Bi Maxine Brown atashughulikia mawasiliano kati ya kamati na watanzania waishio nchini Uingereza kuelekea mkutano huo. 
Orodha ya wajumbe wengine wa kamati hiyo itawasilishwa baadae. Kamati hii itafanya kazi kwa karibu na ofisi yetu ya Ubalozi kufanikisha Mkutano wa Diaspora 2014. 
Kamati inaomba watanzania waishio Uingereza waupe uongozi wa kamati ushirikiano katika kufikia lengo hili ambalo hatimaye ni kwa manufaa ya watanzania wote na maendeleo ya nchi yetu. Ahsanteni. 
(Tanzania-UK Diaspora Task Force) 
26/02/2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...