MTU MMOJA ANAYESADIKIWA KUWA
JAMBAZI SUGU
AMEUAWA NA WANANCHI WILAYANI MOMBA.
MNAMO
TAREHE 09.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:20HRS JIONI MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HEZRON
MWAISANILA (22) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA ALIFARIKI DUNIA WAKATI
ANAPATIWA MATIBABU HUKO KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA BAADA YA
KUSHAMBULIWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA
ZA JADI FIMBO NA MAWE.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA
MAREHEMU HUYO AKIWA NA WENZAKE WAWILI WALIOKIMBIA WALIPORA FEDHA TASLIMU TSHS. MILIONI 1,200,000/=,
ZAMBIA KWACHA MILIONI 1,200,000/=, DOLA ZA KIMAREKANI 60 NA SIMU YA KIGANJANI
MALI YA DENIS ODAS (22)
MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAPOROMOKO – TUNDUMA MAJIRA YA SAA 16:45HRS JIONI AKIWA ANATOKA DUKANI. MAREHEMU ALIKUWA NI
JAMBAZI SUGU NA ALIKUWA ANATAFUTWA NA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO MBALIMBALI YA
UHALIFU LIKIWEMO TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA BAADA YA KUPORA PESA NA
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.675 CLX
AINA YA TOYOTA KLUGER MNAMO TAREHE 25.01.2014
MAJIRA YA SAA 20:00HRS USIKU HUKO
ENEO LA ISYESYE JIJINI MBEYA AKITUMIA SILAHA AINA YA SMG NA KUMJERUHI MFANYABIASHARA
MMOJA AITWAYE OBADIA JANAS (41)
MKAZI WA ISYESYE KWA KUMPIGA RISASI MGUU WA KULIA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE
WATUHUMIWA WA UHALIFU WANAOWAKAMA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA
KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
WATU 7 WASHIKILIWA NA JESHI
LA POLISI MKOANI MBEYA
KWA TUHUMA ZA KUMJERUHI MBUNGE.
MBUNGE
WA JIMBO LA MBEYA VIJIJINI – CCM MHE.
JACKSON MWANJALI (55) ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA RUNGU NA FIMBO KICHWANI NA
KUNDI LA VIJANA WANAODAIWA KUWA NI WAFUASI WA CHADEMA.
TUKIO HILO LILITOKEA
MNAMO TAREHE 09.02.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA
KITONGOJI CHA SHIPONGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKATI MBUNGE HUYO AKIWA NA SHADRACK MWATUNGUJA - KATIBU WA UCHUMI
NA MIPANGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI NA BAADHI YA VIONGOZI WA CCM WA WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI WAKIWA WANATEMBELEA VITUO VYA KUPIGIA KURA KATIKA KATA YA
SANTILYA AMBAVYO VIPO KATIKA JIMBO LAKE.
MTUHUMIWA PAUL WUMBULA (32) MKAZI WA MBALIZI NA WENZAKE SITA WALIKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO. WAHANGA WALIPATIWA
MATIBABU NA KURUHUSIWA, HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA
NA VURUGU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA KAMWE JESHI LA POLISI HALITASITA
KUMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA MTU YEYOTE YULE ATAKAYEJIHUSISHA NA KITENDO
CHOCHOTE CHA UVUNJIFU WA AMANI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
MAELEZO YA HELA HAYAJAKOSEWA KWELI,MILIONI 1,200,000 INAMAANISHA KWA UFUPI M 1,200,000 NA M INAMAANISHA 1,000,000. SASA HII INAMAANISHA KWAMBA NI TSHS 1,200,000,000,000; AMBAYO NI SAWA NA TRILIONI MOJA NA BILIONI MIA MBILI.
ReplyDeleteLAKINI NAFIKIRI HABARI ILITAKA KUMAANISHA NI TSHS 1,200,000; AMBAYO NI MILIONI MOJA NA LAKI MBILI. NAFIKIRI MAREKEBISHO KAMA YANAHITAJIKA YANGEFANYWA KUONDOA MKANGANYIKO NA KUWEPO MAWASILIANO MAZURI, KAZI NJEMA