JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA 
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA NASIBU MWAILUBI (44) MKAZI WA SAI JIJI NA MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 49 SAWA NA UZITO WA GRAM 245. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 19.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA ILOMBA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA  MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU WANAO JISHUGHULISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAFANYABIASHARA 9 WAKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU/ZILIZOKWISHA MUDA WAKE. 

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAFANYABIASHARA 09 WAKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA ZILIZOKWISHA MUDA WAKE. WATUHUMIWA HAO NI 1. JUSTINE GODFREY (28), 2. SALAMA KHALFANI (29), 3. KAJALA GODWIN (35), 4. LAURENCE WINTER (35), 5. VICTORIA CHRISTOPHER (35), 6. ALEX SIMBEYE (25), 7. PHILIPO HERIED (33), 8. ANDREW MWANJALA (35), NA 9. ZUWENA SELEMAN (37). WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA OPERESHENI ILIYOENDESHWA NA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA [TFDA] MNAMO TAREHE 19.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:30HRS ASUBUHI KATIKA MAENEO YA MWANJELWA, ILOMBA, SOWETO NA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. BIDHAA ZILIZOKAMATWA NI PAMOJA NA POMBE KALI [VIROBA] ZA AINA MBALIMBALI, VIPONDOZI VYA AINA MBALIMBALI NA JUICE. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA  MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA/KUSAMBAZA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. PIA ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA BIDHAA ZILIZOKWISHA MUDA WAKE KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU WANAO JISHUGHULISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA ZILIZOISHA MUDA WAKE AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. 

[ROBERT MAYALA – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...