*MTU MMOJA AUAWA KATIKA
WILAYA YA MBEYA.
MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JAPHET
MWANIZUVA (35) MKAZI WA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA ALIFARIKI DUNIA WAKATI
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA MAJIRA YA SAA 06:00HRS ASUBUHI. AWALI MNAMO
TAREHE 01.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:26HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA MAREHEMU ALIJERUHIWA KWA
KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI NA LAITON WILLY. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA
MTUHUMIWA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA NA MKE WAKE SHAMBANI NA ALISHAWAHI KUMUONYA
MARA NYINGI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA. KAMANADA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
*JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WAWILI
WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
JESHIO LA
POLISIN MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. SHIDA GIBSON (29) NA GODFREY
MADOKI (32) WOTE WAKAZI WA KISALASI – MAMBA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] UJAZO WA LITA 3.5. WATU HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.02.2014
MAJIRA YA SAA 12:30HRS MCHANA KIJIJI
CHA KAMABA WILAYA YA CHUNYA KATIKA MSAKO ULIFANYWA NA JESHI LA POLISI.
WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANADA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
*JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
AKIWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA DOLA BANDIA.
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BRAITH MUYUTU (38) MKAZI WA CHINGOLA –
ZAMBIA AKIWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA DOLA BANDIA PAMOJA NA VIPANDE VYA
KARATASI [BLACK DOLLAR] NA VIPANDE VYA
MADINI BANDIA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA TAREHE 04.02.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI HUKO TUNDUMA KATIKA ENEO LA MPAKANI KATI YA TANZANIA NA
ZAMBIA WILAYA YA MOMBA. TARATIBU ZAIDI ZA KISHERIA ZINAFANYWA DHIDI YA MTUHUMIWA. KAMANADA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU/UHALIFU
KATIKA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
*JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LAWASHIKILIA WATU 13
WAKIWA NA BHANGI.
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 13
KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI. KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA TAREHE 04.02.2014 MAJIRA YA SAA 23:00HRS USIKU HUKO KATIKA MTAA
TAZARA – TUNDUMA KELI BULAYA (46)
MKAZI WA MUFULILA – ZAMBIA AKIWA NA WENZAKE 11 WALIKAMATWA NA ASKRI POLISI
WAKIWA NA BHANGI KETE 226 SAWA NA UZITO
KILO 01 NA GRAM 130 PAMOJA NA MICHE
YA BHANGI 120. AIDHA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA ENEO LA IGURUSI STENDI YA
MABASI WIALYA YA MBARALI MOSES ANGOMWILE
(34) MKAZI WA IGURUSI ALIKAMATWA NA ASKARI POLISI AKIWA NA BHANGI KETE 47 SAWA NA UZITO WA GRAM 235.
WATUHUMIWA NI WAUZAJI/WATUMIAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANADA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI
ZA MTU/WATU WANAOLIMA/KUUZA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE.
Signed by:
[ROBERT MAYALA - ACP]
Kny:KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEAYA.
Haya mambo ya wivu wa kimapenzi mbona yamezidi siku hizi..maadili yamekwenda wapi?
ReplyDelete