KWA NIABA YA FAMILIA YA MZEE JOHN ALLONGA WA BUTURI RORYA, NAPENDA KUWAJULISHA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WOTE KUWA BIBI YETU MPENDWA MAGDALENA ONGUKA(MEME) AMEAGA DUNIA TAREHE 5.2.2014 KATIKA KIJIJI CHA BUTURI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 108 MIPANGO YA MAZISHI YANAFANYIKA KIJIJINI BUTURI, BIBI AMEACHA WATOTO WANNE, WAJUKUU 35 NA VITUKUU 42.
TUTAPEANA TAARIFA YA TARATIBU ZITAKAVYOKUWA
Michael G.Allonga
Mjukuu wa Marehemu
Du! Mungu ampumzishe pema. Amefanya alichoagiza Mungu kwa binadamu hapa dunia. Watoto wanne na wajukuu 35!
ReplyDeleteWewe mdau wa kwanza washangaa nini? Au hauishi Tanzania?? Kwa kijijini hao watoto wanne kuzaa watoto kama ifuatavyo unaona haiwezekani: 9 + 9 + 9 + 8??
ReplyDeleteAu ukijumlisha hapo, haupati 35??
Masha Allah, angali anaonekana bado alikuwa na nguvu zake hapo pichani, Mwenyeez Mungu kamjaaliya uzao si haba, kadhalika na umri pia alijaaliwa wa kutosha si haba, kapumzike kwa amani Bibi yetu, MOLA akusamehe kwa yote na kukupumzisha palipo pema peponi - AMEN.
ReplyDeletePoleni sana ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu Bibi Magdalena Onguka Allonga. Mwenyeez Mungu awape nguvu, faraja na stahamala katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Bibi yetu mpendwa.