Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya magazeti yamekuwa yakitoa taarifa za upotoshaji juu ya suala la kuongezeka kwa malipo ya pensheni kwa Waheshimiwa Wabunge. Magazeti hayo yanadai kwamba Mheshimiwa Waziri wa Fedha amethibitisha ongezeko hili.


Taarifa hizo ziliendelea kudai kwamba Waheshimiwa Wabunge watakapostaafu watastahili kulipwa shilingi 160 milioni kila mmoja.

Kwa kupitia tangazo hili, tunaeleza kwamba, Mheshimiwa Waziri wa Fedha hajawahi kuongea na Mwandishi wa Habari yeyote kuhusu suala la nyongeza ya pensheni ya Waheshimiwa Wabunge na maelezo kwamba Mheshimiwa Waziri alithibitisha taarifa za ongezeko hilo sio kweli bali ni maelezo binafsi ya Waandishi wa Habari hizo na suala hilo halipo Serikalini wala Bungeni.

Aidha, tunapenda kuwaasa Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na kuacha kuwachonganisha Wabunge na Wananchi wanaowaongoza kwa kuwapotosha kwa masuala ambayo hayana ukweli na uthibitisho wowote.

KATIBU MKUU – WIZARA YA FEDHA
4 FEBRUARI, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. bila ya shaka katika siasa kuna ulaji nje nje , laa sivyo watu wote wasingekimbilia huko , wasomi wanaacha kazi zao za kitaaluma kuingia kwenye siasa , jee unafikiri ni wakereketwa? thubutu ni fedhaa za wananchi mnazizotumbua bila huruma wala aibu kuwagawana miongoni mwenu , ingelikuwa siasa ni fani ya uzalendo na ukereketwa kwa nini mapato ya wanasiasa yasiwe ya chini kabisa katika nchi? Angalia vile mamilioni ya fedha yanatumiwa kwa sasa kutengeneza viti kule bungeni dodoma , kwani hawawezi kukaa kwenye viti vya kawaida , mbona watoto wetu wanakalia matofali kwa miaka madarasani , wao kwa kikao cha muda wa miezi tu washindwe vipi kukalia vitu vya kawaida? jee mnapopanga hio mishahara minono kwa wanasiasa mnawashauri walipa kodi wananchi?

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwa tamko hili. Lakini hamsemi kama mnapingana na ongezeko la mishahara ya wabunge au la!. Is this just buying time and then later deal hii ikapitishwa quitely wakati masses imeshasahau?
    Tanzania ni Maskini sana jamani. Fedha hizo kwa huruma kabisa kutoka kwa viongozi wangezitumia kuwachimbia wananchi mabwawa katika kila kijiji. Mabwawa yangesaidia kuondoa tatizo la maji, yangeleta lishe bora toka samaki, shughuli za umwagiliaji, recreation, biashara, na beautification ya mazingira. Bwawa is a great investment ambayo it can last for very long. Nyerere angefanya hivyo tusingeishia kuibiwa zile mashine za ku-pump maji za vijiji vya ujamaa. Kijijini ninakotoka yaani maji ni shida; lakini tungepewa bwawa-looo! tungeokolewa mno.
    Kuchochea maendeleo hutokana na kujinyima kwanza na mambo kisha mambo yakinona ndipo starehe.
    Tafadhalini sana jamani wapendwa wetu serikalini muwe na huruma to your poor citizens.Pia muwe openly wakali kwa wanaotaka kujinufaisha binafsi.

    ReplyDelete
  3. Ni vizuri mmetoa taarifa ili kujulisha ukweli.Nahoji chombo/vyombo vya habari vilivyotoa taarifa "isiyo ya kweli" mmevishughulikiaje?Au mnasubiri kesho watudanganye tena...

    ReplyDelete
  4. Tamko sawa lakini mnachukua muda mrefu sana kujibu.uvumi upo wiki sasa na majibu yanatolewa leo.


    mdau wa Bariadi

    ReplyDelete
  5. Mmekanusha! Safi. Ila tusijesikia tena kuwa wabunge wanalipwa kiasi hicho. Imekanushwa na wasilipwe kweli, na sio kukanushwa halafu walipwe chinichini, Noooooooooooooooo!

    ReplyDelete
  6. wale tu,zitakuja kuwaumbua.

    ReplyDelete
  7. Tamko lenu lingekuwa na tija, kama mngesema kuwa ni kweli an siyo kweli kuwa kiinua mgongo cha wabunge kimepanda.

    Sasa kutuambia kuwa Wizara haijasema kuwa kiinua mgongo cha wabunge kimepanda haileti maana yoyote kwa sisi wananchi!

    ReplyDelete
  8. Tamko hata halina maana kwasababu ninavyojua mbunge akimaliza muda wake wa miaka mitano analipwa mafao asilimia 40% ya mishahara yake ya miaka mitano na posho ya 20% ya mishahara yake ya miezi 24,sasa mlivyopandisha mishahara yao moja kwa moja mafao yameongezeka msitufanye kama watanzania wote tumelala au hatuna akili,yaani tumechoka sana na huu ubabe..mtu unasoma kwa shida tena shule binafsi ukija kupata tu kazi unaanza kukatwa PAYE kubwa kama serikali imekusomesha hela yenyewe watu wanakwenda kulipana posho,jamani kuweni na huruma

    ReplyDelete
  9. Uongo mtupu huo, hongera wote mliotoa maoni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...