Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akifanya mahojiano na Mwandishi wa Gazeti la The Independent la Nchini Uingereza kuhusiana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika Vita Dhidi ya Ujangili nchini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) akimtambulisha Mshauri wa Masuala ya Vyombo vya Habari nchini Uingereza Bw. David Tarsh (kulia) kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Benard Membe jijini London, Uingereza wanakohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Biashara Haramu ya Wanyamapori.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Daily Mail la Uingereza Bw. Guy Zitter (kati) na Mhariri wa Gazeti la Mail on Sunday Bw. Geordie Greig (kulia) alipotembelea Ofisi za Gazeti la Daily Mail jijini London, Uingereza kuelezea juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika Vita Dhidi ya Ujangili nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akihojiwa na Mtangazaji wa Idhaa ya  BBC News Day Bola Mosuro katika Studio za BBC World Service jijini London, Uingereza anakohudhuria Mkutano wa Biashara Haramu ya Wanyamapori ambapo alipata fursa ya kuelezea juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika Vita Dhidi ya Ujangili nchini. Picha zote na Pascal Shelutete, TANAPA. 
Habari kamili soma hapo chini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...