Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, imeingia katika Ujumbe wa Bodi Tendaji ya Mashirika na Mifuko ya Umoja wa Mataifa inayosimamia na kuratibu masuala ya Maendeleo, Tanzania ni miongoni mwa nchi 35 zinaounda Bodi hiyo. Pamoja na kuwa mjumbe, Tanzania pia ni Makamu Rais wa Bodi ikiwakilisha nchi za Afrika. Tanzania itakuwa mjumbe wa Bodi kwa kipindi cha 2014 hadi 2016. Pichani baadhi ya Maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu, Bw. Noel Kaganda na Bi. Ellen Maduhu wakifuatilia moja ya vikao vya Bodi ambapo Tanzania ilishiriki.
Sehemu ya wajumbe wakifutaliana majadiliano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...