Mkutano wa nane wa maajadiliano ya wazi kuhusu maandalizi ya malengo mpya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs) umekamilika siku ya Ijumaa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. 
 Katika Mkutano huu wa wa wiki moja wajumbe walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu mada kadhaa ambazo ziliwasilishwa mbele yao kuangalia ni kwa namna gani zinaweza kuwa sehemu ya malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu. 
Mada hizo zilihusu masuala ya Bahari, Misitu na Viumbe hai, Usawa wa Jinsia na uwezeshwaji wa wanawake, uzuiaji wa machafuko, uimarishaji wa amani , ujenzi wa amani baada ya machafuko, utawala wa sheria na utawala bora. 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya Mataifa 30 yaliyokuwa yamechaguliwa kuwa wajumbe wa majadiliano hayo ya wazi ( Open Working Group). na Imeshiriki kikamilifu tangu mkutano wa kwanza hadi huu wa mwisho
Balozi   Celestine Mushy, Mkurugenzi,  Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, akizugumza katika mkutano huo wa mwisho wa maandalizi ya  malengo mapya ya maendeleo  endelevu baada ya  2015, Balozi Mushy ndiye aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika  Mkutano huo. Pembeni ni Bw. Noel Kaganda Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Wajumbe wakifuatiali mchango wa  Tanzania  uliowasilishwa na  Balozi Mushy kuhusu  uzuiaji wa  machafuko,  uimarishaji wa amani,  ujenzi wa amani baada ya machafuko,  utawala wa sheria na utawala  bora.
Sehemu wa washiriki wa mkutano wa mwisho wa maandalizi ya malengo  mapya ya maendeleo endelevu  baada ya 2015
Washiriki wengine wakifutalia kwa makini majadiliano hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. I may be too ignorant of these international processes but why don't I see any specific post MDG proposals in the speech. We have more history than proposals. NGO' s have made specific proposals on health, education and climate change financing. The government does not have any such ideas. I thought this was a process to offer concrete ideas. Where are they?

    ReplyDelete
  2. C'mon Tanzania! U can so better than this. This meeting was called United Nations to receive specific proposals on post MDG development proposals. I have read this speech five times I see no proposals for post MDG. We spend too much time on history and self praise with no substance proposal. nGo's have offered many good proposals on education, health and climate change and good governance. I see none. Does the government have any of its own? Why not state them here in 1,2,3 and 4. The meeting was called to receive proposals instead we offer history and self praise! How can this be? We surprise people!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...