Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ilala, Jesca Njau (kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi wodi ya watoto wachanga Katika Hospitali ya Rufaa ya Amana Ilala iliyokarabatiwa kwa msaada kampuni hiyo, Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali hiyo, Dk. Mtagi Kibatala, Mhandisi wa TBL, John Malisa na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Meshack Shimwela. TBL ilitumia sh. mil. 68 kukarabati wodi hiyo na miundombinu yake.
Jesca Njau akipongezwa na Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali hiyo, Dk. Mtagi Kibatala,
Dk. Kibatala akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo ambao alidai umepunguza kwa asilimia kubwa kupunguza adha kwa wazazi waliozaa watoto njiti. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kazi nzuri TBL! Hawa watoto ndio taifa la kesho na wateja wenu!
ReplyDeleteMdau Canada