KAMPUNI ya Bia (T.B.L) kupitia Brand ya KILIMANJARO imeamua kuliboresha Bonanza la Twanga Pepeta la kila Jumapili linalofanyika katika viwanja vya Leaders Club.

Maboresho hayo ni kutoa Bia moja ya Kilimanjaro kwa kila atakayelipa kiingilio. Licha ya kupewa Bia moja ya Kilimanjaro, kiingilio cha mlangoni kimepunguzwa sana mpaka kufikia Tshs 2,500. 
Kwa kawaida kiingilio cha Leaders huwa ni Tshs 5,000/= lakini TBL imeamua kukipunguza mpaka Tsh 2,500 kwa kuwa italipia mapungufu. 
TBL imeamua kuliboresha Bonanza ili kuwawezesha wapenzi wa Twanga Pepeta na wa muziki wa dansi, kupata fursa ya kukutana kwa pamoja mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kupata burudani ya michezo mbalimbali na hatimaye kuburudika na muziki. 
TBL kwa muda mrefu imekuwa ikiisapoti Twanga Pepeta na kwa wakati wote itaendelea kuisapoti kwa kuwa ni Bendi kubwa Tanzania. 
Ikumbukwe pia TBL ndio muanzilishi wa Mabonanza mengi Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla na kwa kushirikiana na Twanga Pepeta ndio walioanzisha Bonanza la Leaders Club. 
Imetolewa na JESCA NJAU 
T.B.L RETAIL SALES MANAGER.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...