Mganga wa Kituo hicho Dk. Gbson Mbaza alienyoosha mkono  alisema Tbl imetoa msaada mkubwa na muhimu katika sekta ya afya kwa sababu huduma hiyo inahitaji huduma ya maji kwa wingi kutokana na mahitaji ya usafi kwa wagonjwa na mazingira kuhitaji maji mengi.
 Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya TBL, Doris Malulu,
Alisema ili miradi iwe endelevu na imnufaishe mwananchi aliyekusudiwa ni vema suala la uangalizi likawa shirikishi kwa kila mtu ambapo itakuwa misaada kwa vizazi vijavyo na kwamba kampuni hiyo imelenga kituo cha Afya kwa kuwa ndiyo kimbilio la Watu wengi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mdogo wa Tunduma, na pia ni mkaguzi wa ndani  Helen Kagamizi, aliishukuru Kampuni ya Tbl kwa msaada wa kisima cha maji katika Kituo cha Afya kwa kile alichosema Mji wa Tunduma unatatizo kubwa la uhaba wa maji.

KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) imezitaka Halmashauri mbali mbali nchini ambako miradi mingi ya kijamii inatekelezwa kutokana na misaada ya Wahisani kutoa uangalizi ili iwe endelevu kwa manufaa ya wananchi ambao ndiyo walengwa.

Ombi hilo limetolewa na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya TBL, Doris Malulu,wakati akikagua mradi wa uchimbaji wa Kisima cha Maji  uliofadhiliwa na Kampuni hiyo katika kituo cha Afya cha Tunduma kilichopo Wilayani Momba Mkoa wa Mbeya.

Doris alisema maeneo mengi wanapeleka miradi ambayo Serikali ilitakiwa kuifanya ambapo baada ya kufanikisha miradi hiyo na walifadhili kuondoka miradi hiyo hufa kutokana na kukosekana kwa uangalizi toka Serikalini.

Alisema ili miradi iwe endelevu na imnufaishe mwananchi aliyekusudiwa ni vema suala la uangalizi likawa shirikishi kwa kila mtu ambapo itakuwa misaada kwa vizazi vijavyo na kwamba kampuni hiyo imelenga kituo cha Afya kwa kuwa ndiyo kimbilio la Watu wengi.

Aliongeza kuwa msaada wa kisima hicho unagharimu zaidi ya Shilingi Milioni 24, ambapo alisema TBL imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu iliyojiwekea ya kurudisha fadhila kwa jamii kutokana na faida wanayopata kutokana na mauzo ya bidhaa zao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mdogo wa Tunduma, Helen Kagamizi, aliishukuru Kampuni ya Tbl kwa msaada wa kisima cha maji katika Kituo cha Afya kwa kile alichosema Mji wa Tunduma unatatizo kubwa la uhaba wa maji.

Alisema mradi huo utakapoanza kufanyakazi utakuwa mkombozi kwa watu wengi hususani wagonjwa ambao ndiyo wahitaji sana wa Maji na kwa mujibu   Mkandarasi anayechimba kisima hicho anasema kinaweza kuzalisha Mililita 5000 kwa saa.

Naye Mganga wa Kituo hicho Dk. Gibson Mbaza alisema Tbl imetoa msaada mkubwa na muhimu katika sekta ya afya kwa sababu huduma hiyo inahitaji huduma ya maji kwa wingi kutokana na mahitaji ya usafi kwa wagonjwa na mazingira kuhitaji maji mengi.

Aliongeza kuwa maji hayo watayatunza vizuri ili yaweze kuwasaidia katika shughuli za kila siku za matibabu na wagonjwa kutokana na kukabiliwa na upungufu wa maji safi na salama kwa mji mzima wa Tunduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hizi nyasi za kituo hiki mbona hazijakatwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...