Waziri wa Uchukuzi,Mh. Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni mbalimbali waliofika kushuhudia ushirikiano mpya kati ta ya benki ya TIB na Development Bank of Southern Africa (DBSA) baada ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa miundombinu nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TIB Peter Noni akizungumza na wageni mbalimbali walifika kuhudhulia hafla hiyo baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kuendeleza miundombinu nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DBSA Bwana Patrick Dlamini (wa pili kutoka kushoto walio kaa) na Mkurugenzi Mkuu wa TIB Bwana Peter Noni (watatu kutoka kushoto walio kaa) wakitiliana saini makubaliano ya kushirikiana kwa pamoja katika kuwezesha uendelezaji wa miundombinu nchini. Waliosimama nyuma ni pamoja na Mh. Dk Harrison Mwakyembe na Mh. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Fedha.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DBSA Bwana Patrick Dlamini (wa pili kutoka kushoto walio kaa) na Mkurugenzi Mkuu wa TIB Bwana Peter Noni (watatu kutoka kushoto walio kaa) wakikabidhiana hati hizo za makubaliano ya kushirikiana kwa pamoja katika kuwezesha uendelezaji wa miundombinu nchini. Waliosimama nyuma ni pamoja na Mh. Dk Harrison Mwakyembe na Mh. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Fedha.
Miongoni mwa wageni walioalikwa kushuhudia tukio hilo ni pamoja na wajumbe wa kamati ya Bunge ya miundombinu, viongozi mbalimbali wa serikali na makampuni ya umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...