Mshindi wa promosheni ya Timka na bodaboda Bw.
Ramadhani Abdallah akipiga kiki pikipiki yake tayari kuondoka nayo mara baada
ya kukabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Nje Salum Mwalim(kulia) katika tukio
lililofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.
Meneja
uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiongea na washindi wa promosheni
ya Timka na bodaboda iliyomalizka hivi karibuni wakati wa hafla ya makabidhiano
iliyofanyika Makako Mkauu ya Vodacom eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.Jumla
ya washindi 48 walikabidhiwa bodaboda zao zikiwa tayari zimeshasajiliwa.
Sehemu ya pikipiki zikiwa tayari
kutolewa kwa washindi wa promosheni ya Vodacom ya Timka na bodaboda iliyomalizika
hivi punde. Pikipiki hizo zilikabidhiwa kwa washindi katika hafla fupi
iliyofanyika Makao Makuu ya Vodacom yaliyopo Mlimani City jijini Dar es salaam
Sehemu
ya pikipiki 48 zikiteremshwa kwenye viunga vya Makao Makuu ya Kampuni ya
Vodacom tayari kwa ajili ya zoezi la kukabidhiwa kwa washindi wa iliyokuwa
promosheni ya timka na bodaboda iliyomalizika hivi karibuni na kuhusisha wateja
wa Vodacom
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (wa kwanza kulia) akifuatilia zoezi la
kuhakiki taarifa za washindi wa bodaboda wa iliyokuwa promosheni ya timka na
bodaboda iliyomalizika hivi karibuni. (Kutoka kushoto) ni Ofisa Uhakiki wa
Viwango wa Vodacom Ombeni Urasa, Regan Rugangira (mshindi) na Ofisa Masoko wa
Vodacom Prestin Lyatonga. Jumla ya washindi 48 walikabidhiwa bodaboda zao
kwenye hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Vodacom, Mlimani City jijini Dar
es salaam.
Mshindi wa promosheni
ya Timka na bodaboda Bw. Japhet Shedrack akiondoa pikipiki yake mara baada ya
kuhakikiwa na (Kutoka kushoto) Ofisa Uhakiki wa Viwango wa Vodacom Ombeni Urasa, Ofisa Masoko wa Vodacom
Prestin Lyatonga, Salum Mwalim Meneja wa Uhusiano wa Nje. Jumla ya washindi 48
walikabidhiwa bodaboda zao kwenye hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya
Vodacom, Mlimani City jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...