Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Bwana Togolani I. Mavura (pichani) kuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba) kuanzia Februari 8,
mwaka huu, 2014.
Taarifa iliyotolewa Jumanne, Februari 25, 2014, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Bwana Mavura anachukua nafasi ya Bwana
Msafiri Marwa ambaye amehamishimiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na kupangiwa kazi nyingine.
Kabla ya
uteuzi huo, Bwana Mavura ambaye ni Ofisa wa Mambo ya Nje alikuwa Katibu wa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
Wapare watani zangu haoooooo!!
ReplyDeleteTogo,
ReplyDeleteCongratulations.
Always current, with demonstrative research capabilities, and impeccable articulation - that is who you are! Grow it up all and full.
Congratulations Kaka... wewe ni jembe .... ninakufahamu, nilikufundisha, tulifanya wote kazi, .... you are the right Presidential appointee....
ReplyDeleteHongera Togolani
ReplyDeleteMwana wa mfumwa