Na Pamela Mollel,Arusha
Wafanyabiashara hapa nchi wametakiwa kutoendeleza mgomo wa mashine za kieletroniki za EFD’S na badala yake wafungue maduka na kuendelea na biashara zao kwa kutumia mashine kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza masharti ya kufanyabiashara.
Rai hiyo aliitoa jana Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania Rished Bade wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha ambapo alisema kuwa kitendo cha kutumia mashine kwa wafanyabiashara itawawezesha kuweka kumbukumbu sahihi.
Alisema kuwa kodi ya ongezeko la dhamani ilikuwa kwenye awamu ya kwanza hivyo awamu ya pili wafanyabiashara hawatahusika kulipa kodi kama wengine wanavyodai
“siyo kweli kwamba wakitumia mashine watafilisika bali watakuwa na kumbukumbu sahihi…na kuna watu wachache wanapotosha wafanyabiashara kwa hili” alisema Bade.
Aidha aliwataka wafanyabiashara kutokubali kutumika na wasiowafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwashawishi kufunga maduka ili kushinikiza serikali bali wawaripoti katika mamlaka husika ili sheria ichukue mkondo wake
HAPA SWALA LA MSINGI NI BEI KUBWA YA MASHINE IKIWA PAMOJA NA GHARAMA ZA UENDESHAJI WA HIZO MASHINE. LAKINI KUBWA ZAIDI NI KWANINI UKIFUNGA BIASHARA HAUWEZI KIIUZA KWA MTU MWINGINE?
ReplyDeleteAah wapi! Gharama za mashine hizo zimepunguzwa kutoka 1.2m mpaka 600,000/- Isitoshe, kama mfanya biashara angechukua accounting and inventory package, computer/laptop, learning curve, maintenance, internet access etc, wangekuwa wanalipa zaidi ya hizo EFD ambazo kwa laki 6 zinafanya inventory, stock taking, financials zingine, all these a big advantage katika kutunza kumbukumbu za mfanyabiashara anaye tumia hizi!!
ReplyDeleteSomewhere somehow someone is being lied to big time!!